Marehemu Rabbiel Daniel Swai
(7/3/1941 – 3/3/1997)
Ni miaka kumi na saba (17) ya majonzi na huzuni imepita, tangu ulipo tutoka gafla katika maisha ya duniani, siku ya Jumatatu na tarehe kama hii 3 March 1997.
Kama wakristo tunaamini, maisha ni safari na mungu ndiye aliyeamua kuwa wewe upumzike mapema. Pamoja na kuwa umetutoka kimwili, ki roho bado uko nasi.
Unakumbukwa sana na mkeo mpendwa wako Elly Rabbiel Swai, watoto wako wapendwa Doris, Nelson, Clemence, Frank na Edward. Wakwe zako Aikael , Gloria na Tutu.
Wajukuu zako Bradley, Dryden, Deryne, Desmond, Donavan na Ellie Reney bila kuwasahau dada yako Elly Ndosi , ndugu zako wote, jamaa na marafiki wote waliokupenda kwa moyo.
Hakika tunakukumbuka kwa mema mengi uliyotuachia, haswa upendo wa dhati kwa wote, tukiamini ndio taa itumulikayo katika maisha yetu.
Tunamshukuru mungu kwa zawadi ya maisha yako, na kwa miaka mingi ya Baraka tuliyo kuwa pamoja hapa duniani. Tunakuombea mungu baba akupe mapumziko mema mpaka pale tutakapo kutana tena.
Tunakumbuka faraja tunayoipata katika Zaburi ya 123.
Amen.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...