Kwa niaba ya Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea na Mwana hisa wa “VIP Engineering and Marketing Ltd” Mzee James Rugemalira aliyependa kuwa nasi leo lakini akashindwa kutokana na majukumu mengine, tunayo furaha kuwatangazia, kuwa VIP ataanzisha mfuko maalum wa kusaidia katika kuboresha utoaji Elimu katika nchi yetu, utakaoitwa “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust”. Mfuko huu unaanzishwa kwa heshima na kumbukumbu ya mzazi wetu mpendwa marehemu Ma Auleria Kobulungo Muganda.
Mheshimiwa mgeni rasmi, Tunayo furaha kutangaza kwamba shule yetu ya Kajumulo Girls High school ndio itakuwa shule ya kwanza kufaidika na mfuko huu, na leo, VIP kwa niaba ya “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust” imetoa jumla ya TZS 200 million (TZS 200,000,000) kwa ajili ya kuwasadia baadhi ya watoto wasio na uwezo wa kujilipia lakini wana sifa za kujiunga na kusoma katika shule hii.
Baba Methodius Askofu Kilaini nae alitoa neno
kweli huyo ni fr Vistus Mroso au baba askofu Samson Mushemba? tufafanulieni
ReplyDelete