Mkufunzi wa Chuo Chuo Kikuu Cha Elumu Zanzibar Bw Haji Nyange Makame, kwa faida ya wanafunzi wake akiuliza swali Linalo husu Uhifadhi wa Historia ya Wahasisi wote wa Muungano walio shirikiana na Hayati Baba wa Taifa Mwl J.K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume.
Muhifadhi mwanadamizi wa Historia, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni nchini Bi Flower Manase akiwafafanulia wanachuo cha UCEZ Historia ya Muungano.
Mkufunzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Bedda Athanas akiwasilisha Mada ya Historia ya Tanzania mbele ya wanachuo wa UCEZ.
Wanachuo cha UCEZ wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam juu ya biasha ya watumwa hapa Nchini.
Wanachuo na Wakufunzi wa UCEZ wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Na Mdau Sixmund Begashe wa Makumbusho ya Taifa
Taasisi za Elimu nchini zimeshauriwa kushirikiana na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Nchini ilikuwapatia nafasi walimu na Wanafunzi nchini kujifunza kwa Matendo mambo mbali mbali ya Historia ya nchi yao hususani ya nayo husu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rai hiyo imetolewa na Muhifadhi mwanadamizi wa Historia, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni nchini Bi Flower Manase baada ya kutoa semina fupi ya Historia ya Muungano na Faida zake iliyo andaliwa maalum kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar na kutolewa na Bw Bedda Athanas katika Makumbusho hiyo.
Bi Manase aliongeza kuwa vijana wengi wa Taifa hili wamejiingiza kwenye mijadala mingi inayo husu Muungano kwa kufuata maneno ya watu wengine bila wao kuijua historia ya kweli ya Mungano wa Tanzania na kusababisha malumbano ya siyo na msingi.
“Wakati sasa umefika wa Tanzania Bara nao waige mfano wa Chuo kikuu cha Zanzibar wa kujifunza historia ya kweli ya Nchi yetu kupitia machapisho, picha na Video zinazo husu Muungano zinazo patikana hapa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam na kuachana na habari za kishabiki zinazo patikana vijiweni’’ aliongeza Bi Manase.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu wa Chuo Kikuu hicho, Bi Hawa M. Saidiq alisema kuwa amepata nafasi adimu iliyo mpatia mafunzo adhimu ya kimatendo zaidi na kufanya aelewe zaidi yale aliyo kuwa akijifunza darasani juu ya historia ya Muungano wa Tanzania.
Nae Mkufunzi wa Chuo Chuo Kikuu Cha Elumu Zanzibar Bw Haji Nyange Makame alie ongozana na wanafunzi hao, alikishukuru uongozi wa Idara ya Program cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambayo amesema yamezidisha ufahamu zaidi kwa wanafunzi wa Chuo hicho juu ya Historia ya Tanzania hususani ya namna zilivyo ungana.
“Nawashauri wanafuzi na walimu wa Tanzania Bara na Hata Visiwani, kwa kupitia Makumbusho ya Taifa waisome vyema historia ya Tanzania ili wapate ufahamu wa kweli zaidi juu ya Muungano kwani kwa kufanya hivyo itasaidia sana kuulinda Kuueshimu na Kuudumisha Muungano huu tulio nao sasa’’ Alisema Bw Makame.
Wanafunzi na Walimu wa Chuo Kikuu Cha Elumu Zanzibar (UCEZ) wamekuwa wakiitembelea Makumbusho na sehemu mbali mbali za kihistoria hapa nchini ili kujitanua zaidi katika ufahamu juu ya Historia ya Tanzania na Mambo mengine ya nayo husu Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani.
SIASA ndio mzuizi wa fitina katika kupindisha Historia.
ReplyDeleteUkiona Muungano unapingwa jua pana Uenezi wa Kisiasa za Upinzani chini ya mkeka ama nyuma ya pazia!
Hivi Taarifa za Tukio la Mapinduzi ya Zanzibar 12 Januari 1964 hadi kufikia Muungano 26 April 1964 , SASA KUTOKEA MWAKA 1964 HADI SASA MWAKA 2014 ZIMEPITA KARNE NGAPI, ZA KUSEMA HISTORIA IMAPOTEA KUPELEKEA HAKUNA UKWELI ULIOPO HADI WATU TUANZE KOSOMESHANA NA KUELIMISHAN KWA KUSAHAU UKWELI?
Arobaini ya wapinga Muungano inakaribia, dawa yao inaiva ipo jikoni.
ReplyDeleteKatika Mchakato wa Katiba, ile filimbi ikipulizwa pyeeeee!
Katiba imekamilika, hawa WACHACHE jamaa wapinga Muungano (TENA WASIO NA HOJA YA MSINGI NA AKILI SAWA SAWA) watakuwa wanawajibiswha kama wahaini TUTAWAPIGA NYUNDO ZA VICHWA NA KUWAZIKA BAHARINI!!!
Wapinga Muungano, Katiba ikikamilika Kiama chanu kitakuwa kimewadia!
ReplyDeleteHONGERA MAKUMBUSHO YA TAIFA KWA HATUA HII, WENGI TUNAUKAKASI JUU YA HISTORIA YA MUUNGANO, SASA NI WAKATI MUAFAKA WAKUONDOKANA NA UKAKASI HUO. SHIME WANANCHI MAKUMBUSHO IPO KWA AJILI YETU.
ReplyDeleteDu! kweli wa Bongo tupo nyuma, watu wanavuka bahari kujifunza kwetu sisi tumekaa tu!!!! Sikulijua hili mapema.
ReplyDelete