Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kesho (Jumatano Machi 5, 2014) anaongoza hafla inayowakutanisha wanawake zaidi ya 250 kutoka kada mbalimbali wakiwemo wasomi, wake wa viongozi, wajasiriamali, wanasiasa kuangalia mafanikio ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii wa mwanamke hapa nchini.

 Wanawake hao wanakutana chini ya kile kinachoitwa “Connected Women” ya Kampuni ya Vodafone ambapo kupitia hafla hiyo wanawake hao watajadali mchango wa teknolojia ya simu za mkononi na jinsi ilivyobadili maisha ya wanawake hapa Tanzania kupitia miradi inayofadhiliwa na Vodacom Foundation.

“Shabaha ni kujenga daraja kwa wanawake wenye mafanikio kwa umoja wao kujenga hamasa na kuwawezesha wenzao wasio na mafanikio kufikia mafanikio ili kuondoa pengo la utofauti wa jinsia lililopo ndani ya jamii hususani sekta ya elimu, afya, uchumi na uongozi.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Georgia Mutagahywa. 

 Usawa wa kijinsia imekuwa ni ajenda ya muda mrefu katika mataifa mbali mbali duniani ambapo mengi yao wanawake wamekuwa wakinyimwa fursa za msingi ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuleta mafanikio ya kasi kwa jamii husika.

 Mama Salma Kikwete anatarajiwa kuwakutanisha wanawake hawa ambao wamefanikiwa kwa kuwezeshwa kupata fursa za kielimu, kiafya, kiuchumi na uongozi mpaka kuwa watu muhimu na wanaotambulika ndani ya jamii ya watanzania.

 Hafla hiyo inayofadhiliwa na Vodacom ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake dunaini inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.

 Mutagahywa aliongeza kuwa “Wapo wanawake wenye nyadhifa kubwa serikalini, katika sekta binafsi pamoja na mafanikio ya kiuchumi ambapo  kwa umoja wao wakiamua kutumia nafasi walizonazo wanaweza kumkomboa mwanamke mwenzao kutoka katika tanuri la usawa wa kijinsia.”

 Utofuati huu wa kijinsia pamoja na sababu nyengine unachangiwa pia na mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo siku zote zinamkandamiza mwanamke na kumfanya abaki nyuma katika shughuli zote za kimaendeleo huku zikimpa nafasi zaidi mwaname”. Alisema.

Miongoni mwa mafanikio ambayo teknolojia ya simu za mkononi katika kubadili maisha mpango wa M-pesa wa kuwawezesha wanawake mikopo nafuu isiyo na riba – MWEI, mradi wa fistula katika hospitali ya CCBRT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wanawake wa Tanzania wanaweza waamke ili washiriki kikamilifu kusukuma mbele gurudumu la maendeleo nyumbani na katika jamii zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...