Tukiacha mbali picha ambayo mara nyingi au kwa miaka mingi imekuwa ikijengwa  vichwani mwa wengi wanapoona na kudhani kwamba fulani ni kiongozi bora [pengine kwa muonekano tu], au kwa sababu anashuka kutoka kwenye gari kwa mbwembwe, tabasamu baada ya kufunguliwa mlango na mkanda na kisha kupokelewa briefcase yake, yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora na sio bora kiongozi. Na kadri siku zinavyokwenda, taswira ya kiongozi kwa muonekano tu inazidi kupotea. Vitendo,maadili,mafanikio, uvumbuzi na maendeleo vinachukua mstari wa mbele.

Tofauti na miaka ile ambayo picha ya kiongozi bora ilikuwa kama hiyo hapo juu, siku hizi viongozi bora wapo na wanajitokeza katika hali tofauti tofauti kabisa. Anaweza kuwa asiyevaa suti kama Dalai Lama na akawa kiongozi bora. Au asiyevaa suti bali t-shirt na jeans tu kama alivyokuwa Steve Jobs wa Apple au Mark Zuckerberg boss wa Facebook. Mifano ya viongozi hawa ipo mingi.

Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinasema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti, briefcase, tabasamu[ hususani lile la uongo] bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Muandishi nikuulize jee unafahamu nini kuhusu personality na dignity katika uongozi au kuwa kiongozi.Hao wavaaji jeans uliowataja si viongozi maana hao ni wafanyabiashara tuu kwa njia moja au nyengine.Kuwa kiongozi kuna style yake na ndio maana kwa tafiti nyingi zilizofanywa wengi wa viongozi zinapowaponyoka nyadhifa zao huwa hawajisikii vyema kisaikolojia. Muandishi zidi kupembuwa ukweli.Mimi nahisi kama analysis zako,hypothesis zako na theory zako zina kasoro kadhaa.

    ReplyDelete
  2. Hao Mark na Steve uliowaainisha si viongozi ni business oriented persons tu.

    ReplyDelete
  3. Namuunga kabisa mkono muandishi.Uongozi sio uanasiasa tu.Huwezi kusema Steve Jobs hakuwa kiongozi na akaongoza kampuni kama Apple.ni kiongozi yule.uongozi sio ubunge au urais tu.Tuelimike jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...