Pichani Mhe. John Haule akisalimiana na Balozi Teitelbaum katika Wizara ya Nje ya Marekani. Kulia ni Mhe.Liberata Mulamula,Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. John Haule(katikati) katika picha ya pamoja na Mhe.Balozi Donald Teitelbaum(kushoto) na Mhe.Balozi Mulamula (kulia)
Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bw. Michael Morrow, Mkurugezi wa Idara ya Afrika Mashariki baada ya mazungumzo yao katika Wizara ya nje Marekani.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Balozi S.Beattle, Mshauri wa Rais Obama kuhusu US-African Leaders Summit baada ya mazungumzo yao Ubalozini Tanzania House Washington DC.
Mhe.. Balozi Liberata Mulamula (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Beattle(Kushoto) na Bw. Sam Watson (kulia) Msaidizi Maalum wa Balozi Beattle

Kufuatia mwaliko wa viongozi 45 wa bara la Afrika kuhudhuria mkutano wa kihistoria uliopewa jina la US-Africa Leaders Summit utakaofanyika Washington DC,Marekani tarehe 5-6 Agosti 2014, mchakato na mikutano mbalimbali imeendelea kufanyika kuelekea k mkutano huo wa kihistoria ambao Rais Barack Obama atachanganyika na viongozi kuzungumza nao na kuwasikia hoja zao mbali zitakazolenga kuimarisha uhusiano wa nchi hizo na Marekani.

Kwa upande wa Serikali ya Tanzania Mhe. John Haule,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipata fursa ya kukutana na Balozi Donald Teitelbaum, Naibu wa Naibu wa Waziri wa Nje wa Marekani katika Wizara ya Nje ya Marekani hivi karibuni na kuzungumza nae masuala mbali yanayohusu mkutano wa US-Africa Leaders Summit pamoja na masuala mengine ya mashirikiano baina ya Tanzania na Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...