Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.
Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
Mapato hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.

Nayo mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.
Makato mengine bwana yanachekesha sana,hii mechi ni ya CAF,marefa ni wa CAF.Halafu kunakuwa na makato ya CAF na referees wa CAF
ReplyDeleteMilioni 488 zimeingia,jee hasara kwa uharibifu uliotokea ni ngapi na jina la Tanzania nje limepakwa manukato au uvundo.Rekebisheni hii hali wahusika jamani ili jina la Tanzania liwe kioo safi katika medani ya michezo.
ReplyDelete