Hatimaye leo Bunge maalum la Katiba limemchagua Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wake mjini Dodoma.
Hii inakuja baada ya jana kumchagua Mhe.Samweli Sitta kuwa Mwenyekiti. Mhe Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda mpinzani wake Amina Abdalla Amour. Kura 7 ziliharibika - kama jana.
Katibu wa Bunge hilo Maalum ambaye atajulikana wakati wowote kuanzia sasa ataapishwa na Rais Jakaya Kikwete kesho asubuhi Ikulu ndogo Dodoma.
Katibu wa Bunge ndiye atakayemwapisha Mwenyekiti na Makamu wake, na Mwenyekiti atawaapisha wajumbe wote, ndipo shughuli itapoanza rasmi ya kuandika katiba mpya.
Globu ya Jamii inawatakia heri na fanaka katika zoezi hili la kihistoria
![]() |
Mhe.Samia Suluhu Hassan (anaye angalia kamera)akipongezwa na aliyekuwa mshindani wake Mhe Amina Abdalla Amour mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi. |
![]() |
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Bunge
la Maalum la Katiba mteule Dodoma, akishukuru wajumbe kwa kumchagua
|
Wajumbe kinamama wakishangilia mara baada ya Bunge Maalum la Katiba kumpata Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma leo
Hoi hoi na nderemo
Chereko chereko...
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...