Msaidizi wa Willy Matunda akiandaa 'duka' la matunda linalotembea nje ya hoteli ya Zahir katika mtaa wa Mtendeni mjini Dodoma. 
 Willy Matunda mwenyewe akiandaa matunda kwa ajili ya wateja wake. Huyu bwana anasifika sio tu kwa kuwa na matunda fresh kila siku pamoja na usafi bali pia kwa kupania kufanya watu wale matunda sana, sio kungoja hadi mtu alazwe hospitali kwanza ndipo ale...
 Duka litembealo la Willy Matnda 
Wateja kibao kwa Willy Matunda ambaye ameihamasisha Globu ya Jamii kuanzisha safu hii ya kila Jumapili ya NYOTA WA WIKI ambapo watu wanaofanya vyema katika jamii wataenziwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Michuzi mimi ni mkazi wa Dsm nakuja mara kwa mara Dodoma. Nimeiona ubunifu huu wiki iliyopita nikaupenda sana. Ni mfano wa kuigwa. Nimeshakula matunda hapo na nampongeza Willy kwa ubunifu. Usingeiweka hii kwahakika ningekutumia.

    ReplyDelete
  2. Safi sana hii inawasaidia watu kuhakikisha wanakula portion ya matunda inayohitajiwa kwa siku... badala ya kushindilia michips na mihogo kwa lunch. Kaka inabidi uwe unapitia maofisini mida ya lunch watu wanapata fruit salad za nguvu.. well done!!

    ReplyDelete
  3. Nzuri sana.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Ankal kwa safu hii. Binafsi huyo kijana ananipa changamoto kubwa, ni shemeji wa rafiki yangu. Kinachonifurahisha ni kitendo cha kuhakikisha maatunda yanapatikana kwa mwaka mzima ili kuwaridhisha wateja wake. Nimepata stori yake kutoka kwa dada yake. Kiukweli ni mfano wa kuingwa na wengi wetu.

    ReplyDelete
  5. hongera sana ila zingatia vaa mask puani na mdomoni kuzuia mate na hewa, pia vaa gloves za nylon nyembamba mikonono ili kuzuia vijidudud toka mikononi kumbuka matunda huliwa bila kupikwa. ni ushauri

    ReplyDelete
  6. Kijana Hongera sana kwa ubunifu ila kuongeza tu ungejitahidi kidogo kuwa ki afya zaidi kama kuvaa koti spesheli kwa huduma hio na kijikofia cha kuzuia nywele unapokuwa unahudumia wateja.
    ni hayo tu...Hongera sana!!

    ReplyDelete
  7. Hongera bwana Willy kwa ubunifu. Sasa hao wabunge wetu wenye vichuguu vya tumbo wana mahala pa kupata matunda na kujipatia chakula wiano. Tatizo sio Dodoma tena, tatizo ni wewe. Washindwe wenyewe!

    Mdau wa Ng'ambo

    ReplyDelete
  8. nadhani angehitaji avae "white overcoat", "gloves" mikononi, mask (pua + mdomo bilashaka)etc etc.. ni vitu vya muhimu maana hii inahusu moja kwa moja juu ya afya na mustakabali wa maisha ya watu ambao kimsingi ndiyo wateja wa bwana Willy Matunda. Mavazi aina hii yanaonyesha jinsi biashara ilivyo makini pia ikiondoa shaka juu ya afya za wateja; Anaweza pia akatafuta vifungashio (disposable) ili packaging iwe ya ukweli....kivingine, niunga mkono kuwa ni ubunifu wenye weledi....Mungu amfanikishe m-TZ huyu (Willy Matunda)

    ReplyDelete
  9. We mdau hapo juu, ambaye bila shaka umehamia ng'ambo juzi juzi usilete za kuleta. Kwani umesikia Willy Matunda anaingia theatre kupasua mgonjwa hadi avae hivyo?? Tuoneshe picha moja tu ya aina hiyo tukuamini. Nyie ndio WAKUDA wenyewe mnaosemwa. kujifanya kujua kila kitu wakati si lolote. Willy Matunda ni msafi ananawamikono kila wakati na anatumia plastic disposable plates kuhudumia wateja wake. Angalia picha vyema. Kwanza wewe mwenyewe hapo ukitoka kunya onaonesha hunawi mikono leo unabana pua ati gloves na masks.

    ReplyDelete
  10. Uncle hii kitu inanifanya nitamani matunda yaliyoivia mtini ukienda kwenye supermakrket hapa ng'ambo huwezi kupata matunda yanyoonekana vizuri kiasi hiki. Willy matunda big ups your fruit stand looks very good.

    ReplyDelete
  11. OUT OF TOPIC:
    Uraia wa nchi mbili ni majanga kwa nchi yetu nashangaa kuna hadi mawaziri eti wanaupigia debe kwa faida ya nani???kuna mbongo anaeishi ughaibuni kashindwa kuwekeza bongo kweli???hebu tuache utani jamani wabunge wa bunge la katiba wajadili vitu muhimu kwa ajili ya mamilioni ya watz na sio huu ujinga wa uraia wa nchi mbili hauna faida yoyote kwa nchi yetu..

    ReplyDelete
  12. Willy Matunda Ahsante sana na Pongezi sana kwa ubunifu!!!

    Huu ni mfano wa kuigwa kwa Vijana Wajasiriamali ili kuepekana na Usumbufu wa Mamlaka za Mijini kama Manispaa.

    ReplyDelete
  13. Ama kweli Willy Matunda umeitendea haki Dodoma kwa kufanya biashara kwa Kanuni za Usafi na Sheria huku ukiheshimu ya kuwa Ndio Makao ya Serikali.

    Ni jukumu la Manispaa Dodoma kuchukua utaratibu huu kwa mji mzima kulinga na Koti kubwa la heshima ambalo mji wa Dodoma umelivaa kwa kuwa Makao Makuu ya Serikali.

    ReplyDelete
  14. Bravoooo.... Willy, Hio ni FURSA endelea kujituma....

    ReplyDelete
  15. OUT OF TOPIC: Kweli huko nje' ya topic, pole sana. Naona uko na harakati kali sana za kuukata huo uraia pacha. Pole sana. Kukujibu siyo kila mtu aliye Ughaibuni ana uwezo wa kuwekeza. Jamani Ughaibuni siyo mbinguni kwamba unapata pesa kirahisi. Vile vile uwezi ukalazimisha watu wawakeze, ni hiari yao. Na mtu anapowekeza anategemea atapata faida, na mie navyoijua Bongo wekeza halafu uondoke uone faida yake. Jamani najua Bongo kwetu shule ni ngumu lakini tuache kutegemea vitu vya kirahisi raisi tu. Mwisho, mie sitaki uraia pacha kwani ni kahsifa nyingi. Lakini najua hao mawaziri na wakuu unaowasema wameamua hivyo basi itakua hivyo. Kwani watoto wao wengi wansoma huku, wewe baki uanpiga kelele za kijinga tu. Sasa hivi ni geresha toto tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...