Mkutano wa vyama vya kijamaa ulimwenguni - Kamati ya Afrika umeonza Leo jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere , mkutano huo utamalizika kesho.
baadhi ya wawakilishi wa CCM katika mkutano huo wajumbe wa NEC , Ndg. Magesa kushoto na Balozi Karume kulia.
Baadhi ya Wajumbe wa secretariat na wajumbe wa mkutano wakibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CCM Dar es Salaam Ndg. Madabida wa pili kulia na Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya kijamaa Ndg. Ayala wa pili kushoto wakati wa mapumziko.
Wawakilishi kutoka nchi mbali mbali za Afrika wakishiriki katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hatuja hama moja kwa moja kutoka wenye Siasa ya Ujamaa!

    Sasa ndugu zetu Majuu mnataka Pasipoti mbili, hivi Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Suala la Pasipoti mbili wapi na wapi?

    Kwa kuwa mlisha vunja sharia ya Uraia 'Breaching Citizenship Law' kwa kukana Uraia wa Tanzania, Sheria haija badilika kwa vile Sheria haijaenda likizo mkirudi Mtakamatwa Mtakwenda Lupango miesi 6 mkitoka ni Mafunzo ya JKT na Mgambo miezi 6 ndio mrudi Kundini kama Watanzania na mkiwa na Uraia wa nchi moja Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

    Je, mpo tayari kwa kifungo cha miezi 6 na Mafunzo ya miezi 6 ya Mujibu wa Sheria huku mkirudi ktk Uraia wa nchi moja Bongo Tambarale?

    Hatuna Jinsi msimamo wetu kwenye maamuzi mengi kama Suala la Uraia Pacha unategema Siasa ya Ujamaa kama mnavyoona Siasa ya Ujamaa ndio hiyo inawekewa Vikao hapo!

    ReplyDelete
  2. mdau #1,pole sana kama ulinyimwa hizo visa, Diaspora hawako kwenye huo uamuzi. Maana naona una hasira sana kwa ndugu zako wa Ughaibuni. Wewe ukichoka jiwekee kitanzi tu, jamaa wa Diaspora wanakuja Bongo kila siku bila kujali kelele zako, kwani wako kutafuta maisha, siyo kama wewe unayetegemea kuwanyanyasa wenzio kwa vitisho. Pole sana.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Pili:

    Madiaspora wana tabu ya maisha>

    Wao ndio wanao hangaika kutaka Pasipoti yetu na Uraia lakini sisi hatuna shida na Pasipoti yao wala Uraia wao.

    Hata mimi huwa ninaenda Majuu na kurudi kam kawaida na Visa napata.

    Pia (nakuandikia kwa herufi kubwa hapo chini nikitoa msisitizo kwako wewe kumuunga mkono Mdau wa kwanza Mbongo wa Pasipoti moja kama mimi)

    NASEMA HIVI: ''FEDHA NIMEZIPATA HAPA HAPA NCHINI KWA JAKAYA KIKWETE BILA HATA KUVUKA MPAKA WALA KUPANDA NDEGE, NIKIENDA MAJUU NINAENDA KUTUMIA NA HUWA NARUDI NYUMBANI NCHI YA AHADI JAKAYA KIKWETE LAND''

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...