Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo (NHIF) wakiwa katika Mkutano wa kujadili umuhimu wa wa huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na kuangalia namna ya kuzindua rasmi mpango wa kuchangia kabla ya kuugua katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya jana Mjini Matai. Katika salamu zake za ufunguzi alizitaka halmashauri Mkoani Rukwa kuhakikisha kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyake vyote vya maamuzi, Aidha alizitaka Halmashauri ziandae utaratibu wa kuzitambua familia zisizo na uwezo wa kuchangia na zitenge fedha kutoka katika vyanzo vyake ili kuzilipia familia hizo na kuhakikisha kuwa hakuna mkazi wa Halmashauri husika anapoteza maisha kwa kukosa fedha za kuchangia katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mwanachama wa mfuko huo anatakiwa kuchangia Tsh 10,000/= kwa mwaka ambao ni mchango wa kaya moja isiyozidi watu sita.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Filbert Ngaponda (Mwana wa Magreth) akiwatambulisha washiriki wa Mkutano huo wakiwepo watendaji wa Serikali na madiwani wa halmashauri hiyo pamoja na wageni mbalimbali waalikwa ambao ni wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (CHF).
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia washiriki wa mkutano huo.
Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Hamza Temba wa pili kushoto akiwa na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NHIF) Mkoa wa Rukwa mara baada ya Mkutano huo.
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Rukwa wakijadili jambo kuhusiana na huduma za mfuko huko. Kulia ni Ramadhan Juma Ofisa Habari Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo, Hamza Temba Ofisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na Ndugu Mussa Hajj Chewa Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo
Picha ya Pamoja ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, viongozi wa Serikali, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Watumishi wa ofisi hiyo Mkoa wa Rukwa. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...