Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Tohara kwa wanaume Mkoani Rukwa iliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi. Akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya Mkuu huyo wa Wilaya amesema hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu 2014 Mkoa wa Rukwa unatakiwa uwe umeshafanya tohara za wanaume 22, 000 ikiwa ni agizo la kitaifa ambapo hadi sasa jumla ya wanaume 7,000 wameshafanyiwa tohara.  

Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo Mkoani Rukwa tangu kampeni hiyo ianze tarehe 17 Machi 2014 hadi jana tarehe 20 Machi 2014 jumla ya wanaume 583 wameshafanyiwa tohara ndani ya siku 4 katika kituo kilichopo tarafa ya Challa. Kampeni hiyo inaenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU ambapo kati ya wananchi 699 waliopimwa ni mmoja tu amekutwa na maambukizo ya virusi hivyo katika tarafa hiyo ya Challa.

Akizungumzia faida za tohara kwa wanaume amesema husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi  pamoja na kusaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiwasalimia wananchi wa tarafa ya Challa waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akizungumza katika hafla hiyo. Akizungumzia juu ya zoezi hilo la tohara amesema tohara kwa wanaume husaidia  kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%. 
Zoezi la Tohara likiwa linaendelea katika zahanati ya Challa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa awasalimu wananchi wa Challa.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha (watatu kulia), Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Albinus Mugonya (wa tano kulia) na watumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ebo!

    Mwanaume kutahiriwa na Mwanamke inakubalika?

    Ahhh, hapana bora kama ni Mpango wa Tohara nitachukua Kisu kikali sana nijikate mimi mwenyewe 'soksi' langu kuliko kukatwa na Ngariba mwanamke!!

    ReplyDelete
  2. Makubwa!

    Enheee, yaani mwanamume nilale chali nikatwe 'zoba' langu na mwanamke?

    ReplyDelete
  3. Raisi Kikwete Dodoma jana kwenye Hutuba yake amezungumzia baadhi ya 'rafu' ktk Katiba kama ukomo wa Uongozi ktk ngazi ya Ubunge hii kitu haifai!

    'RAFU' nyingine ninayo iona katika Mpango huu wa Tohara wa Kiserikali ni kitendo cha mwanaume kutahiriwa na mwanamke, hii pia haifai nadhani Raisi Kikwete angeona taarifa hii ya 'Shughuli ya Jando' hili hapo pia angezungumzia kwenye Hotuba yake Dodoma jana!

    ReplyDelete
  4. Sisi ndio sisi, tunaweza kuoleana !

    Ina maana huyo Mwanaume anayetahiriwa na mwanamke hapo itakuwaje endapo anataka kuoa ndugu wa huyo mwanamke anayemtahiri?

    Si itakuwa ni fedheha kubwa sana kwa jamaa mwanamume hata ile tu kupeleka barua ya posa kwa Ukoo wa huyo mwanamke anayemtahiri?

    ReplyDelete
  5. Mbona watu mna mawazo bado ya mfumo dumeeee????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...