Na Abdulaziz Video,
Kilwa
Moto umeteketeza nyumba anayoishi mkuu wa wilaya ya Kilwa,
mkoani Lindi, Mhe. Abdallah Ulega na kusababisha hasara kubwa ambayo idadi yake
haijaweza
kufahamika mara moja.
Habari kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Katibu tawala wa mkoa
wa Lindi Bw. Abdala Chikota alisema kwamba moto huo umeteketeza
vifaa mbalimbali ndani ya nyumba ya kiongozi huyo.
Bw. Chikota alisema moto huo umesababisha hasara kubwa.
Alisema kufuatia tukio hilo ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa fedha
Shilingi laki tano 500.000 pamoja na chakula kama mchele, unga sukari,
mafuta ya kula pamoja na maharage ili kumsaidia DC huyo katika kipindi
hiki cha majonzi wakati utaratibu mwingine wa kutatua
tatizo la makazi yake ukifanyiwa kazi.
Mkuu wa wilaya huyo, Mhe. Ulega, alisema kuwa vitu
vichache tu ndiyo vimeweza kuokolewa, ambavyo vilikuwa
rahisi kuchukuliwa ikiweno begi la nguo na nyaraka zake, na kwamba kwa
sasa atalazimika kuishi katika jengo la Hostel.
Mhe. Ulega ameshukuru juhudi za wananchi ambazo zimesaidia kuokoa vitu
vichache, vikiwemo seti ya
makochi, magodolo matatu na kitanda kimoja cha mbao
Amesema wakati nyumba yake ilipokuwa ikiungua, familia yake akiwemo mke
alikuwa safarini na amerejea leo mchana.
Kwa upande wake kamanda wa polisi Regnal Mzinga amethibitiasha kutokea
kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo
cha moto huyo
mkuu wa wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, Mhe. Abdallah Ulega (mwenye tracksuit ya bluu) na majirani wakiwa nje ya nyumba yake iliyoteketea kwa moto asubuhi ya leo
Sehemu ya uani mwa nyumba hiyo
Sehemu ya ndani
Nyumba hiyo kwa mbele
Sehemu ya ndani ya nyumba hiyo
Haya matukio ya moto yamezidi, kama yakizidi tutahitaji kuwa na fire extinguisher kila nyumba sasa.
ReplyDelete