Afisa Habari wa TASAF (mwenye T-SHIRT NYEUPE) Estom Sanga akizungumza na mmoja wa wanafunzi ambao kaya yake inanufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo ambao kaya zao zimo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani Bunda mkoani Mara.
Samweli George na Anna George ambao wanatoka katika kaya inayonufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini wakiwa makini kuelekea shuleni.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mcharo ambao kaya zao zimo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini wilayani Bunda mkoani Mara.
====== ===== ====
Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umewezesha mahudhurio ya wanafunzi katika shule za msingi kuimarisha kwa kati ya asilimi 80 hadi 100.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea baadhi ya shule ambako wanafunzi wanaotoka katika kaya masikini ambazo ziko katika mpango huo ,wamesema mahudhurio ya wanafunzi kwa sasa ni mazuri hali iliyochangiwa kwa kiwango kikubwa na uboreshwaji wa huduma wanazopata baada ya kaya zao kuingizwa katika mpango wa kunusuru kaya masikini.
Hivi sasa wanafunzi ambao walikuwa wakikosa masomo kwa kukosa vifaa vikiwemo sare,madaftari,kalamu na hata viatu kwa sasa wanahudhuria masomo yao bila matatizo na hata uelewa wao umeelezwa kuongezeka tofauti na kabla ya mpango huo kuanza.
Miongoni mwa masharti ambayo kaya masikini zilizoingizwa kwenye mpango wa kuzinusuru ambao unaratibiwa na TASAF ni kuhakikisha kuwa watoto wa kaya husika wanahudhuria shuleni na hata kupata huduma za lishe na matibabu pale wanapoyahitaji.
Hawa madaktari, marubani na mainjinia wa kesho.
ReplyDelete