Mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya mashariki jana ulishiriki Tamasha la michezo katika ukumbi wa Dar Live kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuchangia damu na kuendesha zoezi la kuchangia damu kwa hiari.
Tamasha hilo liliandaliwa na kuratibiwa na klabu ya Magenge ishirini na mianzini kwa kushirikisha klabu mbalimbali kama last jogging, Temeke family, kingugi, Respect na nyingine nyingi. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Global publisher, PSPF, Akiba Commercila Bank na Damu salama ambapo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Angela Kizigha Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki ambaye aliongozana na Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dr Faustine Ndugulile pamoja na Diwani wa keko Bwana Noeli.
Tamasha hilo lilikuwa na malengo yafuatayo:
Kuchangia damu kuisaidia kuondokana na changamoto ya upungufu wa Damu katika hospitali za serikali na binafsi.
kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana kama ukosefu wa ajira na madawa ya kulevya, kuleta umoja, mshikamano na undugu baina ya vijana kupitia michezo na kuburudika na kufurahi kwa pamoja kwani ni sehemu ya maisha.
Akijibu risala ya klabu ya magenge ishirini, Mgeni rasmi aliwashukuru kwa moyo waliouonyesha wa kuandaa tamasha ambalo lina lengo la kukutanisha klabu mbalimbali na kuchangia damu kwa hiari na pia aliahidi kuwazawadia shilingi milioni moja na nusu ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za klabu, pia mbunge wa kigamboni mheshimiwa Dr Faustine ndugulile aliwazawadia shilingi milioni moja na diwani wa keko Bwana Noel alitoa zawadi ya shilingi laki tano.
Katika Tamasha hilo Jumla ya chupa za damu 90 zilikusanywa ambazo zitapimwa na kusambazwa katika hospitali mbalimbali jijini Dar-es-salaam.
Mbunge wa kigamboni mheshimiwa Dr Faustine ndugulile pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika mashariki Mheshimiwa Angela Kizigha wakichangia damu.
Mmoja wa washiriki wa Tamasha la michezo akipimwa wingi wa damu kabla ya kuchangia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...