Na Richard Bagolele 
Mradi wa kutibiti gugumaji kanda ya ziwa chini ya ufadhili wa wa mradi wa hifadhi ya mazingira ya ziwa Viktoria awamu ya pili (LVEM II) umetambulishwa rasmi wilayani Chato.
 Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwennye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mratibu wa mafunzo hayo Bw. Emanuel Kitabo amesema lengo la kutambulisha mradi huo kwa wadau mbalimbali wa Chato ni kuhifadhi na kutunza mazingira ya ziwa Victoria vikiwemo vyanzo vyake ardhi oevu na madakio yake. 
Bw. Kitabo Amesema lengo la kuandaa mafunzo hayo ni pamoja kuweka mfumo rahisi wa kupeana habari za udhibiti na ufuatiliaji wa shughuli za gugumaji, kuweka mfumo endelevu wa utafutaji raslimali pesa kutekeleza sheria ya udhibiti wa gugumaji ya mwaka 1999 pamoja na kuimarisha jamii kudhibiti gugumaji kibiolojia na kwa kutumia mikono. 
Amesema njia rahisi ambayo jamii inaweza kutumia katika kudhibiti gugumaji ni pamoja na kutumia wadudu aina ya Mbawakavu ambao hushambulia gugumaji, njia nyingine ni kuondoa gugumaji kwa njia ya mkono na kudhibiti shughuli za kilimo kandokando ya ziwa. 
Akichangia katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Chato ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye mafunzo hayo alishauri kuundwa kwa klabu kwa kila kijiji cha kupambana na udhibiti wa gugumaji. Wajumbe waliohudhuria mafunzo hayo wamesema ni lazima jamii ipewe elimu ya uharibifu wa mazingira ikiwemo kilimo kandokando ya ziwa na vyanzo vya maji. 
Diwani wa kata ya Bwongera Mhe. Batholomeo Manunga amesema kuna kila sababu ya kusimamia sheria za ujenzi holela kandokando ya ziwa Victoria na uthibiti wa uvuvi haramu kupitia kamati za udhibiti wa mialo (BMU).
Naye diwani wa kata ya Muganza Bw.Marco Maduka amesema suala la udhibiti wa gugumaji linatakiwa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi Wilaya. 
Mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Desemba2013 ambapo mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Simiyu na Kagera itahusika katika mradi huo.
Mradi utaandaa dodoso la ukusanyaji wa takwimu za shughuli za udhibiti wa gugumaji, kufundisha wataalamu wa kutumia dodoso la ukusanyaji wa takwimu kukusanya takwimu, kubaini maeneo yaliyoathiriwa, vikundi kazi na kuvijengea uwezo wa kudhibiti gugumaji pamoja na kuhimiza Halmashauri kutenga bajeti na mfumo endelevu wa upatikanaji wa fedha kugharamia shuguli za udhibiti wa gugumaji. 
Gugumaji ni mmea uotao kwa kuelea majini na ni mmea hatari kwa viumbe vya majini ambao hustawi kutokana na taka kutoka viwandani, majumbani na kilimo kandokando ya ziwa. 
Mmea huu kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ulionekana mto sigi mwaka 1955 na baadae mto Pangani mwaka 1959 na mto Kagera mwaka 1985,
 Mratibu wa mafunzo ya udhibiti wa gugumaji Bw.  Emmanuel Kitabo akieleza lengo la mradi kwa wadau mbalimbali wa Wailaya ya Chato
 Mtaalamu kutoka LVEMP Emanuel Kitabo akionesha kwa wajumbe mdudu aina ya Mbawakavu ambaye hushambulia gugumaji
 Mtoa mada wa LVEMP Bw.Fred Kanuti Akionesha kwa wadau wa mafunzo tofauti ya mumea ulioathiriwa na mdudu aina ya Mbawakavu ambaye hushambulia gugumaji na mmea ambao haujaathiriwa na Mbawakavu
Wadau mbalimbali wakifuatilia mafunzo ya udhibiti wa gugumaji ziwa vivtoria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...