
Pichani wa tatu kulia ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Sistyl Nyahoza akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Ruaha International,mkoani Iringa kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la kalenga, ikiwa ni pamoja na Sheria ya gharama za Uchaguzi kwa wagombea na vyama husika vinavyoshiri katika Uchaguzi huo utakaofanyika machi 16 mwaka huu.Shoto ni Bwa.Mihayo Kadete,Erald Martin na kulia ni Isaya Makoko ambao wote ni Maofisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano uliondaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga mapema leo asubuhi,na pia Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa kujitambulisha uwepo wake katika zoezi zima la uchaguzi wa Kalenga sambamba na kuwafahamisha Wananchi zinazofanywa na Ofisi za Msajili wa vyama vya siasa tangu Maafisa wa Ofisi hiyo wafike mjini Iringa.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akifafanua jambo kwa Wanahabari
Nje kidogo ya mada:NGOME IMARA YA KALENGA-Kuna somo moja shule ya msingi tulisoma(sisi wazee!) hii habari ya Kalenga(Historia? darasa la 4,5,6?Can't remember) mambo ya Mkwavinyika.
ReplyDeleteNa kinachoendelea bunge la Katiba ndiyo nini sasa??Ni aibu aibu......
David V
Kweli waikumbukia historia. Nami nikukumbushie kidogo. Hapo Kalenga ndipo palipokuwa makao makuu ya Ntemi Mkwawa. Na baada ya kupambana na wajerumani kwa miaka 4 na kujikuta amebakiwa na wafuasi wachache wapiganaji na keshazungurukwa na wajerumani,basi hakupenda akamatwe yu hai isipokuwa alichokifanya ni kujiripua kishujaa kukwepa mateso ya walowezi wa kijerumani. Hata hivyo wajeru walikikata kichwa chake na kukipeleka Ujerumani katika makumbusho yao.Na baaada ya uhuru siku kupita ndipo Wahehe wakakidai na kupewa na kukizika rasmi kwa heshima zote . Kinachoendelea Bungeni si aibu isipokuwa ni kuchafuka kwa bahari tu katika safari ni jambo la kawaida.Na kwa mantiki hiyo basi "KUGOWA au KUTAPIKA" au hata kuhisi kizungu zungu ni kawaida tu.Lakuomba hili jahazi livuke salama na kutia nanga salama katika bandari ya makubaliano.
ReplyDelete