Kikosi cha Yanga 
 Kikosi cha Al Ahly
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri akitafuta namna ya kumzuia katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
 Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akitafuta namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Al Ahly ya Misri katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
 Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akizuiwa na Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri,Ramy Abdel Aziz katika Mchezo wa Mashindano klabu bingwa Barani Afrika,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Yanga imeshinda bao 1 - 0.
Kipa wa timu ya Al Ahly ya Misri,Sherif Ekramy Ahmed akida moja ya hatari iliyokuwa ikielekeshwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ama kweli Yanga Bunduki!

    Yaani dk. 45 zimepita bila kufungwa?

    Nafikiri wana Jangwani wakikakamaa Kiume wanaweza kuwalisha Pilau , Tende na Halwa Wamisri!

    ReplyDelete
  2. Nakataa,Yanga hawakuwafunga Al Ahly,Yangu wamewafunga Mabingwa wa Afrika!Mara ya mwisho hawa kufungwa na Timu ya Tanzania ilikuwa mwaka 1985 CCM na Simba(2-1),magoli ya Zamoyoni Mogella na Mtemi Ramadhani wakati huo niko shule ya msingi,sikumbuki mechi ya marudiano ilikuwaje lakini Simba hawakuvuka.

    Niwapongeze mashabiki wa Simba,pamoja na kuwashangilia wapinzani lakini ushangiliaji hauwa kama tuliouzoea(ulipungua sana),tunaelekea kuzuri.Kwa timu za kutoka nje ya Tanzania,tuweke unazi pembeni.ANGALIZO KWA YANGA;Mechi ya marudiano Al Ahly watakuwa "Mnyama mwingine tofauti" na tuliyemuona jana.

    David V

    ReplyDelete
  3. MASHABIKI WA SIMBA ACHENI KUSHANGILIA TIMU ZA NJE KITAIFA. MUWE WAZALENDO NA MJIUNGE NA WATANZANIA WOTE KUSHANGILIA NA KUUNGA MKONO TIMU YA TANZANIA INAYOCHEZA NA TIMU YA NJE YA NCHI. UTAIFA NI MUHIMU SANA.

    HONGERENI WANAJANGWANI KWA KAZI NZURI KUMFUNGA BINGWA WA AFRICA -AL ALHY.

    ANGALIZO-YANGA PANGENI MIKAKATI UZURI. HAWA MABWANA WAMEONDOKA NA MAUMIVU MAKUBWA. HAWATAKUBALI KIRAHISI KUFUNGWA NYUMBANI. UWEZO WA KUWAFUNGA BADO MNAO-TENA MKUBWA. SAFU YA USHAMBULIAJI, NOENI MASHUTI YENU. BADO UMALIZIAJI SI MZURI SANA.

    MUNGU AWABARIKI-MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  4. Yanga sasa moto wa kuotea mbali. Mna nafasi ya kuwa funga hawa mabigwa, hata kwao.

    ANGALIZO:-
    Safu ya ushambulizi fanyieni kazi MAKOSA ya jana. Mmekosa nafasi nyingi mno.

    Mungu awabariki wana Jangwani na Watanzania wote. Mungu ibariki TANZANIA.

    Tawa KPR-Dar

    ReplyDelete
  5. Yanga wajiandae kisaikolojia na kimchezo maana watafanyiwa kila aina ya vitimbi wakati WA mechi ya marudiano ndani na nje ya uwanja.
    Mhifadhi

    ReplyDelete
  6. Yanga wawe makini sana. Waarabu wana hila nyingi sana.

    Pia Yanga wana tabia ya kubweteka pindi wanapotangulia kupata goli hasa ugenini. Wasipokuwa makini watafumgwa magoli mengi tu.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Yanga ila kumbukeni Kawaida ya Timu za Misri ugenini ni kutafuta sare au kufungwa magoli kidogo ili mechi ya marudiano kwao wamalize shughuli. Inabidi kufanya matayarisho ya kutosha kuwakabili kwa namna yoyote kule kwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...