Habari kutoka Madison Wisconsin nchini Marekani zinasema kuwa mtanzania, Michael Agustine Lukindo (pichani), amefariki Dunia na hakuna taarifa zozote kuhusiana na ndugu zake. Lukindo ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Tanga ameacha mke na watoto wanne.
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, Oliver Temba  juhudi za kuwapata ndugu zake hazikufanikiwa. Marehemu Michael Lukindo amefariki dunia mjini Madison Wisconsin-USA, kutokana na hali hiyo familia ya marehemu imewaomba ndugu wea marehemu kujitokeza au kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za kupatina kwa ndugu zake ajitokekeze.

Kwa mujibu wa Oliver, mazishi ya marehemu Michael Lukindo yatafanyika siku ya Jumamosi na mwili wake utachomwa moto, marehemu Michael Lukindo amekuwa akiishi Marekani kwa zaidi ya miaka 30 na ameacha mke 'African amerika', na watoto wanne.

Mungu ailaze mahali pepa peponi roho ya marehemu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. pengine Michael Lukindo sio jina lake halisi, watu wakija huku ugaibuni wanabadili majina alafu hawawajulishi ndugu zao kwamba wamebadilisha majina.Kama hapa Uk Wazanzibar kibao wamebadilisha majina.Makaratasi yanasumbua sana ndonama watu wanajikuta wakidanganya majina.
    Mdau London.

    ReplyDelete
  2. Message ya awali ilipata ndugu na namba zao za simu za Tanzania

    ReplyDelete
  3. Ni huzuni kubwa kwa mtanzania mwenzetu kufariki dunia.

    Hata hivyo ndugu zetu wa Marekani hivi kiswahili kimewapotea au vipi? taarifa inajigonga, aidha jamaa zake hawakupatikana au hawajulikani?

    Kutopatikana sio kutojulikana. Kutopatikana ni ukosefu wa mawasiliano baina ya wanaotafutwa na wanaotafutwa.

    siamini kuwa hawajulikani, mkewe hata kama ni wa african america atakuwa amewahi kumsikia mumewe akiwazungumza jamaa na ndugu zake waliopo nyumbani na hata nchi nyengine.

    Ni vibaya na inauma kufikiria kuwa marehemu hakuwa na mawasiliano na ndugu na jamaa zake nyumbani kwa miaka yote alioshi huko marekani na miaka yote baada ya kuwa na mke na watoto.

    ReplyDelete
  4. RIP UNCLE MICHAEL

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa,
    Nina maswali mawili tu kuhusu huu ujembe, Marehemu ana familia yake huko ughaibuni, miaka yote hiyo, je hakuwahi kuwasiliana na familia yake bongo? Mke, je, ndugu za mmeo hukuwahi kumuuliza, miaka 30? Wana Diaspora kweli kweli mnatuchanganya na jinsi gani mnavyoishi huko, mnawasahau ndugu zenu, lakini kwenye kilele cha maisha mnatutafuta.

    Swali la pili, nadhani hili ni kwa Michuzi blog managers, mazishi ya kuuchoma mwili ni jambo la kawaida tu sehemu nyingi duniani, mlivyoandika message sidhani kama inaashiria kuwa hii ni kawaida, au pengine mngetafuta neno/jina kamili la hii, na sio "mwili wake utachomwa moto"

    Rest in Peace Oliver Temba

    ReplyDelete
  6. Mungu amuweke mahali pema peponi!Je hakuwa na marafiki wa kitanzania huko Marekani?Mpaka kuenda huko akiwa mtu mzima atakuwa kapita shule,kaishi mitaani huku Tanzania.Je uhamiaji hawana takwimu zake za hati ya kusafiria?Dunia ya leo ni ndogo sana kwa hiyo kuna utata wa suala hili,kuna Warundi,wazaire,wamalawi wengi ambao wanasafiria hati za Tanzania zenye majina ya kitanzania.Kwani huyu hakuondoka zamani lazima angetambulikana tu.

    ReplyDelete
  7. NDUGU YAKE ANAITWA SALIM LUKINDO ANAPATIKANA TANGA MJINI NAMBA YAKE NI 0684498169

    ReplyDelete
  8. Hao ndugu wanatafutwa ili wafanye nini kama akiwa hai hakuwai yeye kuwatafuta sasa Leo majivu yake yatawasaidia nini hao ndugu. Kwa nini ndugu wanatafutwa? Timu ya blog maagizo ya kutafuta ndugu yanatoka wapi?
    Kama mke hukuwatafuta ndugu wakati wa uhai wa mume leo wa nini?

    ReplyDelete
  9. Mdau #5, Kwanza kabisa, Namwombea kwa Mungu ampuzike pema peponi Ndugu Lukindo. Pili mdau#5 maswali yako ni ya kijinga, unapouliza, "miaka yote hiyo, je hakuwahi kuwasiliana na familia yake bongo?" Hivi maiti inaweza kukujibu?(na wakati wa kilio si wakati wa kuongea ujinga) na mawazo kama yako unadhani ndugu yako anaweza kuwa na moyo wa kukutafuta? Halafu wewe unasema wakati wa kifo ndiyo wanakutafuta. Hivi wewe umesoma hii habari?!! Hapa kweli marehemu anatafuta ndugu zake au watu walio hai? Kwa mawazo kama haya ndiyo maana hatufikii mbali jamani. Tusemage ukweli, maiti haina haya. Na hii ndiyo hali halisi. Endeleni tu kuongea pumba, sijui waliukana uraia, sijui wanajidai, na dharau nyingi(wabeba maboksi), mwisho tutavuna tulichopanda. Na sasa haivi mnawakatalia ndugu zenu huo uraia pacha, ambao na nyie sio wenu, sasa mnadhani watapata moyo wa kuwasaliana na nyinyi? Ndugu Lukindo mie naona alikuwa amejipanga vizuri tu. Kwani kabla ya kupumzika alishasema anataka mwili wake uchomwe na hii ni kupunguza gharama za kurudisha mwili Bongo. Na unaposema labda alikuwa awasiliani na ndugu, ni kweli inawezakana kuwa hivyo, maana kwa kauli za fitina, wivu, na uongo wabongo wachache wanazotoa kwa ndugu zao wanaDiaspora sasa hivi inawezakana zilimkatisha tamaa. Marehemu ana shida, yeye kampuzika najua labda ndugu zake(watoto na mke), ambao ni haki yao wanataka kujua ndugu zao wa TZ, lakini sasa kwa kauli kama zinazotolewa humu labda ndiyo maana marehemu akutaka ata kujuna na ndugu zake. Ndiyo maana inabidi tupiganie uraia pacha. *Mmbongo Chiberia*

    ReplyDelete
  10. Mi nna ndugu ambaye tangu aondoke in 80s hatujui yuko wapi. Alienda kusoma bulgaria kisha miaka ya 90s akaonekana us chicago. Hatuna taarifa zaidi ya hiyo licha ya kufuatilia sana ubalozin na kwingineko. Sishangai la huyu!

    ReplyDelete
  11. Jamani mlio nje muwe na mawasiliano na ndugu zenu no excuse, miaka 30?yaani ukoo mzima ata mkeo Kama ni Mmarekani asimjue ata ndugu Mmoja?Rip mike.

    ReplyDelete
  12. Huyu jamaa mnasema hana ndugu huko ni kumlalilisha marehemu si meonyesha familia yake kubwa kabisa mke watoto wanatodha kabisa na marfiki kumsindikiza ktk safari yake ya mwisho hao ndugu mnaowataka ni utaratibu tu lakini kwa kipindi hiki kigumu kilichoamuliwa kuchomwa kuzikwa ni matakwa ya hiyo familia aliyokuwa anaishi nayo. Nyie ndugu zangu onyesheni ungwana kidogo ktk kutatutua mambo ya namna hii utaratibu mliotumi kuweka kwenye mtandao sio mzuri. Be polite and concern

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...