309253_4514172497095_415944777_n Mwanamuziki wa Injili aliyetokea kwenye familia ya kidini Milka Kakete anasema alianza kuujua na kuufahamu muziki kwa kina tangu akiwa mdogo, kwani familia yake ni ya kikristo na amepata malezi ya kuwa karibu na kanisa siku zote. Milka ambaye ni mkazi wa Canada na familia yake akiwa ni mama wa watoto watatu na familia yake anaeleza kuwa anaipenda sana familia yake na anajaribu kuweka sawa maisha ya familia na uimbaji wa Injili. Hivi karibuni alitembelea idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) hapa Washington Dc na kupata nafasi ya kufanya mahojiano na idhaa hiyo , Milka ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na jinsi alivyoanza kuimba, nafasi yake katika jamii na familia na pia kueleza vipaji vyake vingine alivyojaliwa na Mungu ikiwa ni pamoja na ushauri wa masuala ya ndoa. 377775_10150398388657143_147606451_n Alipoulizwa juu ya uchungaji Milka alicheka na kusema huo sio wito wake ila yeye anamtukuza Mungu na kueneza neno lake kwa nyimbo za Injili halikadhalika kutoa ushauri kwa wanandoa. 1531893_10202902547349401_931031973_nSikiliza wimbo wake wa Injili nakung'ang'ania  
Milka Kakete pia alifanya mahojiano na VOA kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa. http://www.voaswahili.com/content/article/1866954.html 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...