Mwana-Diaspora Boniface Makulilo alipokuwa katika 
Jeshi la Maji la Marekani (Navy)
Mtanzania Boniface Makulilo ametumikia Jeshi la Maji (NAVY) hapa Marekani kwa miaka miwili na sasa ni mwanajeshi mstaafu (Veteran)
Amezungumza na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kuhusu maisha yake ya jeshini na namna ambavyo watu toka nje ya nchi wanaweza kunufaika na mafao yaliyopo jeshini.
Ameeleza mengi ya manufaa ambayo wengi hatuyajui kuhusu maisha katika jeshi hilo. Karibu uungane nasi
NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa wana-Diaspora wa Afrika walio NJE na NDANI ya bara la Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Madiaspora US wanaona heri wafie na migizo ya maboksi migongoni wakibeba maboksi kuliko kweda vitani!

    Wengi huko Marekani wanaona ni kheri wabebe maboksi kuliko kuingina Jeshini NAVY na AIRFORCE kuogopa labda watapelekwa Iraq, Syria, Somalia ama Afghanistani !!!

    ReplyDelete
  2. Naamini hizi nchi za magharibi USA na UK utaratibu wao haziruhusu mtu kujiunga na jeshi lao mpaka wakupe uraia wao sasa kama ni hivyo naomba mtufahamishe huyu jamaa atakuaje mtanzania?????

    ReplyDelete
  3. Uraia pacha ukiruhusiwa tu basi wewe tunakuchagua kamanda wa Kiksosi cha wanamaji pale Kigamboni .. jitahidi

    ReplyDelete
  4. Uraia pacha tukiuruhusu tumikwisha maana mamluki watakuja na kuingia ktk kila nafsi nyeti za uslama Tanzania.

    Nchi nyingi za Magharibi kina mama wenye watoto wao wakiume hawataki vijana wao wajiunge na jeshi wkapigane vita vya utata nje.

    Hivyo serrikali hizo za nchi za magharibi zinaamua kuwa na programme mahsusi kuruhusu ma-diapora/wabeba-box/wazamiaji kujiunga na majeshi yao.

    Mfano Ufaransa kuna French Legion hapo watu kibao, Uingereza GURKA, USA kama ktk taaarifa n.k huruhusu vijana-wa-kuja kujiunga kwa ahadi kibao kama uraia-wakupewa, sponsorship za elimu, kupata 'maujuzi' ktk fani kama u-chef,kuendesha magari ya kijeshi, helikopta n.k

    Hii inawezesha kupata nguvu-kazi jeshi kwa vile wazawa hawataki kujiunga jeshi kwa lazima -draft-national-service n.k Ila huweza kupata wazawa toka familia masikini pia kwa ahadi kemkem nilizotaja hapo juu.

    Imekuwa kipindi hiki kimerushwa kuweza kujua kuwa ktk Ma-diaspora wenzetu wengine wametumika ktk vyombo vya ulinzi na usalam nje ya nchi yetu ya Tanzania.

    Mdau
    Pasipoti-Moja-Tu

    ReplyDelete
  5. Kama kuna siku USA inapingana na Tanzania kiasi cha kutokea vita, huyo popo atakuwa upande gani!

    ReplyDelete
  6. Natoa wito kwa wale woooooooooote wanaodharau kazi na baadhi ya wana diaspora, mnapotaja kazi zao msisahau kutaja na mishahara yake. Mnapothaminisha kazi zenu pia tajeni na mishahara yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...