Hili ni ghorofa la chuo kikuu UDOM alipojirusha mwanafunzi huyo toka ghorofa ya pili.
Muonekano wa ghorofa hilo alipojirusha mwanafunzi huyo.
======  ====  ====
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24, Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na paji la uso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote  kujibu shitaka la kujaribu kujiua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. This is sad, but these young people sometimes cant cope with stress and pressures of life.Pole bwana mdogo. Jambo lingine napenda kusema kama nguru hata ukimsafisha kwa malimao bado atanuka tu.Sisi miaka nusu karne baada ya uhuru bado tuna harufu za ukoloni.Angalia hapo juu...Jina s/o,miaka, muhaya.

    ReplyDelete
  2. Angewasiliana na wahehe wampe mbinu nzuri za kujimaliza!

    ReplyDelete
  3. Sasa Kamnada Misime, si mmesha thibitisha kuwa Ni Pombe zilimsababishia maamuzi hayo?

    Kwa nini tena muuburuze kwenye Sheria?

    ReplyDelete
  4. Michuzi rekebisheni Mitaala ya Elimu nchini tokea Elimu ya Chekechea hadi Chuo Kikuu ama sivyo tutazika sana kwa watu kujiua baada ya Kufeli masomo!

    Kamugisha, aslihangaa jinsi alivyo soma kwa kukesha na miguu kuiweka ndani ya beseni lakini Maksi alizopata Mtihani uliopita ni sawa na namba za viatu!

    Hivyo akajaribu kuki Bipu Kifo ili Mtihani ujao akifeli akitoe moja kwa moja Ahera!

    ReplyDelete
  5. Kamugisha hajazoea Kufeli Masomo, ktk Ukoo wao asiye na elimu ana Digrii 2 sasa ameona baada ya Pepa lililopita alichemsha !

    Huyo Babu yake Kijijini analima shambani kwenye ndizi na kahawa lakini ana MBA zake 2 kibindoni!

    Hivyo akaona anywe halafu ajaribu Tiketi ya kuzimu kama atafeli tena Masomo Mtihani ujao maana anaogopa Kijijini Bukoba atachekwa sana akifeli!!!

    ReplyDelete
  6. Dogo alikuwa ana bip, watu hujitupa ghorofa 5 kwenda mbele!

    All in all nakumbuka enzizetu tulikuwa karibu sana na ma academic advisers/Councillors, hawa walikuwa wanatusaidia sana katika maisha ya darasani na nje ya darasa. Nikiangalia wimbi la uwingi wa wanafunzi katika vyuo sijui kama utaratibu huo unafanyika ipasavyo. Vijana kwakweli wanahitaji msaada..............

    ReplyDelete
  7. Ankal unawachokoza wahaya

    ReplyDelete
  8. Vijana mkiwa na usongo wa mawazo ongea na watu acha kufikiria eti ndio mwisho wa maisha. Ushauri nasaha wa ndugu au rafiki unaweza kukupa mtazamo mzuri wa maisha au hata suluhishi la tatizo lako. Acheni mambo ya kukata tamaa na maisha wasiliana na wenzako au ndugu wa karibu. Ukisikia shida za wengine pengine utaona zako si kitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...