picha ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo, katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti  wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo.
 Mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm

Na Woinde Shizza,Arusha



Jumla ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti  wilayani Arumeru  kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani  wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo mwenyekiti wa   vijana wa  CHADEMA wa kata hiyo .

tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.



Akiongea wakati wa kurudisha  kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya CCM,Mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa   ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.



Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani CHADEMA  ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli  ambayo inatakiwa iwenacho kama chama



Alisema kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi  na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atakaeweza kukisemea chama  .



Aidha alibainisha kuwa katika kata yao  tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi  bila kufanya maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa.Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi  ya kata yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.



Kwa upande wake  katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa  wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika ofisi ya mkurugenzi  kufuatilia swala hili.



Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka  na kata yao haitapata viongozi wazuri.



Aliongeza kuwa haiwezekani kuchagua viomgozi waizi maana mwisho wa siku wanaoumia ni wao wananchi kwani viongozi wao watakula fedha zao na wao wataendelea kufaidi huku wao wakiwa wanaendelea kuumia ukuwengine watoto wao wakilala njaa.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ama kweli siasa za Tanzania ni vichekesho, kila leo wanachama wanahama kutoka chama kimoja kwenda kingine, yaani wanabadili vyama zaidi wanavyobadili viatu au makoti

    ReplyDelete
  2. Watu wanaingia kwenye vyama kufuata maslahi fulanifulani! Wakiyakosa kwenye chama kimoja wanahamia kingine hadi ndoto zao zitimie. Ki ukweli hakuna anayeingia kwenye chama kwa nia ya kuleta maendeleo (a.k.a. mabadiliko).

    ReplyDelete
  3. Vijana 100 waliokuwa Chadema wametumia akili sana kufanya uamuzi huu.

    KWA KUWA NI WAZI CHADEMA INA KWENDA MWENDO WA ALI JOJO!

    ReplyDelete
  4. Si hilo tuu na wala bado,itafika wakati na hata vyama wasivithamini tena na chini ya katiba mpya kama kitapita kipengele cha wagombea binafsi rukhsa basi vyama vitadoda mana vyama vingi havina ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...