ndege nyingine ya air tanzania aina ya CRJ-200 ER yenye uwezo wa kubeba abiria 50 imeingia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa toka shirika hilo ndege hiyo itaanza kuruka kesho.
Home
Unlabelled
ndege nyingine ya atc yatua dar es salaam, kuanza kazi kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
The mdudu,hebu acheni na utani weni,tushachoka na hatutaki mtuletee visangarara tunataka madege makubwa kama mavocha yakibeba yamebeba sasa ndio nn videge vya watu 50 tu?,kama tunaweza kujenga mjiport mkubwa huko bagamoyo tunashindwa vipi kununua mijindege ya maana ili nasisi tuwazibe midomo ya majirani hasidi,viongozi wa shilika la air Tanzania ndugu zangu muamke kwenye usingizi mzito wa mchana kweupe mliongoze shilika kwa uzalendo wa hali ya juu na muwe na wivu wa kimaendeleo endelevu,mkumbuke hii ni karne ya 21 hatutaki mwendo wa kinyonga tunataka mwendo wa chui au chita.aibu kwenu viongozi wa air Tanzania mshindwe nyie na maisha yenu na wala sio shilika letu..maana mnanenepa nyie shilika letu linakonda,mm nataka nyie ndio mkonde shilika letu linenepe.
ReplyDeleteNimekuwa najiuliza hii biashara inalipa au prestige??? Maana kama mashirika makubwa kama BA wanahaha kwa nini sisi tunashikia bango swala la kuwa na ndege za Taifa....najiuliza kibiashara zaidi na hali ya uchumi wa nchi yetu....
ReplyDeleteMaana isije kuwa tumeongeza mrija...
kama hailipi kwani ni lazima???
Serikali tengeneza viwanja vingi vya ndege na ipe ATCL Pesa kusafiri kwenye hizo new routes then utaona ATCL ikifanikiwa zaidi na haiwezi kuja kufa kamwe.
ReplyDeleteInaweza ikalipa kabisa kama tuna strategy nzuri. Hapa tanzania hata soko la ndani bado sana. Lakini tukumbuke kuwa hapa ndipo palipo na kila kitu hasa vivutio vya utalii unawezabeba watalii toka corner mbali mbali za Ulimwengu na ukapata faida hasa. Angalia Ethiopia walivyo mbali ktk eneo hili
ReplyDeleteKama Mdau wa 4 anavyosema naungana naye kwa kusema ''HAPA NDIPO KILA KITU KIPO'' na hivyo panaumuhimu suala la usafiri wa ndani likaboreshwa.
ReplyDeleteSerikali ipo sahihi kabisa kuliinua Shirika na kuhakikisha kunakuwa na National Flag Carrier hata kama inaonekana Kibiashara hailipi lakini hii ni long term strategy kwa matumizi ya huko tunakokwenda kulingana na majaaliwa tuliyo kuwa nayo hasa ktk suala la RASILIMALI ZA TANZANIA '' HAPA NDIPO KILA KITU KIPO''
Jamani Tanzania imebarikiwa kuwa na
1.Gas LNG Futi za Ujao 43 Trilioni ambazo ZIKIBADILISHWA KUWA MAJI MAJI ni sawa na Mapipa 7.5 Bilioni (WAKAT UGANDA MAFUTA YO NI PIPA 3.5 BILIONI INA MAANA GESI YA TANZANIA WINGI WAKE NI MARA 2 YA MAFUTA WALIYOPAT UGANDA TENA GESI NI NISHATI YENYE KIWANGO CHA CHINI ZAIDI CHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA LESS CARBON EMISSION ENERGY)
2.URANIUM nyingi tu.
3.DHAHABU ,TANZANIA NI Y 4 KTK AFRIKA KWA UZLSHAJI WA DHAHABU.
4.MALI ASILI NA MSITU, TANZANIA INA SPECIES NYINGI ZA MALI ASILI NA VIUMBE PAMOJA NA MAAJABU 4 KATI YA 7 YA DUNIA YAPO TANZANIA.
5.KUTOKANA NA NO.4 HAPO JUU TANZANIA INA ATRACT WATALII WENGI KUJA KUTEMBELEA ABAPO NCHI INAINGIZA USD 1.2 BILION KWA MWAKA KWA WATALII.
6.TANZANIA INA KILOMETA NDEFU ZAIDI ZA MWAMBAO WA BAHARI KTK AFRIA YA MSHARIKI HIVYO BAHARI NA MWAMBAO ZINAVUTA SANA UTALII NA UWEKEZAJI KAMA TUNAVYOONA SHGHULI ZA UTAFUTAJI WA GESI NA MAFUTA.
7.TUNAJIWEKA SAWA KIUSHINDANI KWA KUWA NA HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA ZA UHAKIKA ILI KUVUTA UWEKEZAJI NA MAENDELEO.
8.UHAKIKA WA USAFIRI WA ANGA UNABORESHA USALAMA WA NCHI NA UFANISI WA KAZI.
9.USAFIRI NA MAWASILIANO NI MOJAWAPO YA MAENDELEO.
10.TANZANIA NDIO CENTER OF GRAVITY, KAMA MNAVYOONA DUNIA NZIMA INAITAZAMA ZAIDI TANANA KTK NCHI A AFRIKA, TUNAONA WTU WANAPIGANA HUKO KWAO VIKAO VINAWGHARIMU AKINA KIKWETE NA SERIKALI YA TANZANIA KUTOA SULUHISHO, TUMEONA MWAKA 2013 JANA WAGENI WA DUNIA NZIMA MARAISI NA WAKUU WANCHI ZA DUNIA WAKIWASILI MAGOGONI KWA MHE.JAKAYA KIKWETE KIKAZI NA KIHARAKATI.
HIVYO KWA SABABU HIZO (10) HAPO JUU NI MUHIMU KWA GHARAMA YEYOTE ILE TANZANIA IKASIMAMA KUHAKIKISHA INAKUWA NA SHIRIKA LA NDEGE LINALOBEBA BENDERA YA NCHI.
HIVYO SERIKALI INAFANYA KITU SAHIHI HATA KMA HAIONEKANI KAMA KUNA MASLAHI YA KIBISHARA KWA SASA, HII NI KWA MALENGO YA BAADAE (STRATEGIC PLANNING) NA MIKAKATI YA KIUCHUMI KWA SISI TULISOMA UCHUMI TUNFAHAU.
Hongereni kwa kujikongoja nilodhani mtakua na orser maalum kama ndege tano hadi kumi including wide body sasa hii ndo nini kama Tz inataka kupiga hatua ktk watalii then we need to be serious tuanza na sisi kiruka guanghzou na Hong Kong bangkok na kwingineko
ReplyDeleteHii Biashara ya ndege Tanzania haikusudiwi kwa wewe Damumbaya Kalamaka kueza kusafiri kwenda Mkoani kwenu nchini!,,,wewe utapanda Mabasi na Malori ya Mkaa ya Fuso.
ReplyDeleteHatuangalii faida ya kila tripu ndege ikiruka, tunatazama uakisi wa huduma za ndege kwa kuongeza kasi ya kukuza Uchumi, tazama hivi sasa Utalii inaingiza USD 1.25 Bilioni kwa mwaka na hapo hatuna Shirika lenye ufanisi la ndege je, unafikiri ATCL ikiimarika hilo pato la USD 1.25 Bilioni litabaki hapo hapo?,,, ni lazima litapanda na pia hata Sekta zingine zitaigiza mapato zaidi kwa kuweo Usafiri murua.
Huduma ya Usafiri huu wa ndege Serikali inauboresha ili iweze kiutoa Fursa kwa Wawekezaji na Watalii watakao fika nchini na kuweza kuiweka Tanzania ktk Ushindani kuweza kukuza Uchumi na kuvuta Watalii kwa kasi zaidi kwa Ushindani wa eneo la Afrika ya Mashaiki na Dunia.
Viongozi wa serikali wenye kufikiria hayo myasemayo wana hisa zao huko Precision Air; huwezi kukuza ATC (competitor)!
ReplyDelete