Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto) na Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha Msata,Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa Lugoba,Chalinze.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akiambatana na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chalinze (CCM),Saleh Mpwimbwi (kushoto) pamoja na Msafara wake wakielekea kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakishiriki kwenye dua ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kisomo cha kumuombea Marehemu ambaye ni Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman (alieketi nyuma ya mgombe) mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mrisho Issa na Kassim Msakamali waliokuwa wana Chadema wametumia ile kitu inaitwa Akili za ziada.

    Unapoona unabishana na Ukuta wa Zege yaani mtu ambaye ni Kada wa CCM Mwandamizi Ridhiwani ni sawasawa na zoezi la kupiga ngumi ukutani hapo kitu ambacho utaumia bureee!

    Jaamaa wamepiga bonge la bao kuingia CCM!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...