Wananchi wa kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama,Iringa Vijijini wakinyanyua mikono yao juu kumuunga mkono Mgombea Ubunge jimbo la kalenga,Ndugu. Godfrey Mgimwa.Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16 siku ya jumapili.
 Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,kwa ajili kuzisikiliza sera za mgombea Ubunge wa Jimbo la kalenga,Ndugu Godfrey Mgimwa,uliofanyika kwenye kijiji cha Ilandutwa,kata ya Mgama Iringa Vijijini
 Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bw. Godfrey Mgimwa akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Ilandutwa kata ya Mgama Iringa vijijini, akiendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni ambapo amewaomba wananchi wa vijiji hivyo kumkopesha imani yao na kumpa kura za ndiyo siku ya Machi 16,Jumapili ijayo ili aweze kuwalipa maendeleo katika jimbo hilo.
 Diwani wa kata ya Mgama Bw. Denis Lupala akipiga magoti kumuombea kura kwa wananchi mgombea Ubunge wa CCM Bw. Godfrey Mgimwa.
 Baadhi ya Wanahabari wakiendelea kuchukua matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bi mkubwa Mgombea Ubunge wa Chadema Kalenga fanya maamuzi yenye akili kabla huja umbuka mbele ya Godfrey Mgimwa!

    Tafuta Banda zuri la kupikia Mama Ntilie ujitoe kwenye kugombea Ubunge na mapema ukaanze kazi mpya na maisha mapya!

    Angalau Matokeo ya Uchaguzi yaki tangazwa utakuwa umesha rudisha Mtaji wako kwa biashara ya chakula uliyo fanya kwa wateja wapiga Kura wakati wa Uchaguzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...