Mwenyekiti wa NMB Business
Club Kanda ya Temeke Bw. Ezekiel Matimo Gutti akiongea machache kuhusu
NMB Business Club Wilaya ya
Temeke tangu kuanzishwa kwake.
Mtoa mada kuhusu kodi
kutoka kampuni ya ‘Tanscott Taxation Service Ltd’ Bw. Hirji Abdallah akielezea
kuhusu ulipaji wa kodi wakati wa semina ya wajasiriamali iliyondaliwa na benki
ya NMB .Semina hiyo ulihudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 wa NMB Business Club
kutoka Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Temeke hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Mwanachama wa NMB Business Club Wilaya ya Temeke Bibi
Pili Matimbwa akichangia mada wakati wa semina hiyo.
Meneja wa NMB anayeshugulikia
Mikopo Midogo Midogo Mashaga Changarawe akiongea na wateja wa NMB katika semina
hiyo ya wajasiriamali iliyoandaliwa na benki ya NMB.
Mwenyekiti wa NMB Business
Club Wilaya ya Ilala Bw. Henri Ignas Mrema akielezea jinsi wana NMB Business Club Kanda ya Kinondoni walivyonufaika na klabu hiyo tangu
kuanzishwa kwake na wanavyoendelea kufurahia huduma na bidhaa kutoka benki ya
NMB. Akitoa shukurani kwa niaba ya wanachama wake kwa uongozi wa benki ya NMB
kwa kuandaa semina ambazo zinatoa mafunzo yanayowajenga wanachama wa NMB
Business Club.
Mwenyekiti wa NMB Business
Club Wilaya ya Kinondoni Bw. Ramadhani Njiku akielezea mafanikio waliyoyapata
wanachama wa NMB Business Club Wilaya ya
Kinondoni tangu kuanzishwa kwake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...