Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzania Bw. Yasunori Onishi (kulia) akielezea kuhusu watalaam wa kujitolea kutoka nchini Japan  walivyofanya kazi hapa nchini katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
 Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wake hapa nchini, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. 
 Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akitoa zawadi kwa Mtaalamu wa kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu kutoka Japan Bw.  Jun Tsuda (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita wa kujitolea kutoka nchini Japani iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzanian Bw. Yasunori Onishi.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kulia) akitoa ufafanuzi wa maswali kutoka kwa waandishi wa habari baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani (kushoto) akijibu maswali ya Mwandishi wa Habari wa gazeti la  Daily News Bi. Hilda Mhagama baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...