Wakati Watanzania, katika miaka ya karibuni wamekuwa wakijitahidi kuboresha maisha yao hususan katika suala zima la ujenzi wa nyumba zilizo bora na za kisasa, upande wa pili wa harakati hizi umekuwa ni wa changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi katika kuzifikia ndoto zao hizo, hasa kwa upande wa gharama za vifaa vya kufanikisha ujenzi huo, lakini pale ambapo wameweza kujitahidi kuweza kufikia gharama hizo.


Katikati ya sintofahamu hii, kumekuwa na Watanzania ambao wamekuwa wakijitahidi kuwaza ni namna gani wataweza kuwasaidia wananchi wenzao katika kukabiliana na changamoto hizo, ambapo miongoni mwao ni wamiliki wa kampuni ya Mega Woodcraft Products (T) Ltd, kampuni ambayo imelenga kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya ujenzi nchini kwa kutambulisha mfumo wa kisasa wa ujenzi.

Kifupi, Mega Panel, ni Mega Panel ni polystyrene (EPS) iliyoimarishwa kwa wavu wa chuma cha pua uliopakwa zinc na kuunganishwa kwa nguvu ya umeme ili kuwa kiini cha mkingiko wa waya zilizopenyeza kwenye polystyrene ambapo polystyrene iliyochomekwa katikati ya wavu wa chuma cha pua huzuia moto na umeme na ingawa panel hii ni nyepesi ina sifa ya kuifanya iwe kifaa cha ujenzi imara na kinachodumu. 

Inaweza kufungwa na kujengwa haraka na ni imara kuliko matofali au matofali yenye uwazi.Mfumo huu wa ujenzi ilianza Marekani, licha ya kuwa kitu kigeni nchini, lakini umeshatumika katika nchi kadhaa na kuonyesha mafanikio makubwa nchi kama Japan, China ,Korea, Afrika Kusini, Msumbiju, Botswana na ata majirani zetu Kenya wanatumia mfumo huu wa ujenzi ,

Manufaa ya ujezi huu ni ujenzi mwepesi na rahisi, hutumia asilimia hamsini (50%) tu ya ujenzi ukilinganisha na ujenzi wamatofali, hupunguza asilimia thelathini (30%) ya saruji , hupunguza gharama za usafirishaji na unajenzi (installation cost), haitaji msingi mkubwa kwa sababu Mega Panels ni nyepesi sana ukilinganisha na matofali hivyo ni rahisi kuongezea gorofa (Vertical extension),  kutoka kwenye nyumba ya chini ni rahisi kujengea maumbo maalum (design configuration), imara sana kutonana na wavu wa chuma cha pua (wire mesh reinforcement), hupunguza joto kwa asilimia ishirini(20%) kutokana na polystyrene, pamoja na mambo yote hayo  mfumo huu ni rafiki wa ikolojia.

Aidha, paneli hizi ambazo zinapatikana katika ukubwa wa aina mbalimbali kwanzia ukuta wa nje (load bearing wall) ukuta wa ndani (pattion wall) dari (roof panels/ slab panels) kwa ukubwa wa 1.2 mtrs X 2.8 mtrs), zimethibitika kuwa pia na uwezo wa kuhami bamba, ukuta na hata paa, pale zilikotumika, huku pia zikiwa na uwezo wa kuhami sauti, kuhami msingi na vitu vingine vingi. 

Ili kujua zaidi kuhusu mfumo huu, wasiliana na Mega Panels kupitia tovuti yao www.mega.co.tz , ikiwa ni pamoja na mbinu za ujenzi wake nk. na ikiwa bado una maswali zaidi, unaweza kuwatembelea Mega Woodcraft Products (T) Ltd ofisini kwao, mtaa wa Bungoni, kiwanja namba 508, au kwa barua pepe jonathan@mega.co.tz Tel: 0787 621 918.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Teknolojia mpya za vifaa vya ujenzi zitaapunguza gharama na kuharakisha upatikanaji wa makazi bora na ya kisasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...