Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa maji wa Mkonze katika Maanispaa ya Dodoma katika kilele cha wiki ya maji leo Machi 22, 2014. Kushoto kwake ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kulia kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe lamsingi la mradi wa maji wa tangi la maji la Chuo Kikuu cha Dodoma ikiwa ni moja ya shughuli za kilele cha wiki ya maji
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtwika maji, Bibi Edna petro baada ya kuzindua mradiwa maji wa Mkonze katika Manispaa ya Dodoma ikiwa ni moa ya shughuli za kilele cha wiki ya maji
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa tangi la maji ikiwa ni moja ya Shughuli za kilele cha wiki ya maji leo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipita ndani ya bomba kubwa la maji katika maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazohusiana na maji yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma kabla ya kutoa hotuba ya kufunga wiki ya maji leo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...