Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitizama sehemu ya mbele ya kiwanda cha kutengenezea Konyagi feki ambapo muonekano wake ni maduka na saloon. |
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitembelea sehemu ya nyuma ya kiwanda cha kutengeneza Konyagi feki katika eneo la kambi ya raha Bomang'ombe wilayani Hai. |
Sehemu ya bidhaa zilizokamatwa katika kiwanda hicho zikiwa kituo cha polisi Bomang'ombe. |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha Pombe feki ya Konyagi iliyokamatwa hivi karibuni wilayani Hai |
Kamanda Boaz akiwa ameshikilia sehemu ya malighafi zinazotumika kutengezea Konyagi Feki. |
Kamanda Boaz akionesha mihuri ambayo imekuwa ikitumika kuonesha tarehe ya kuanza na kumalizika kwa tarehe ya matumizi ya kinywaji hicho. |
Kamanda Boaz akitizama Ndoo kubwa maarufu kama Diaba ambayo yamekuwa yakitumika kuchuja pombe hiyo kabla ya kuwekwa katika karatasi maalum. |
Hivi ndivyo inavyoonekana pombe hiyo ikiwa na alama ya TRA. |
Baadhi ya
watuhumiwa waliokamatwa baada ya kukutwa wakifanya shughuli ya
utengenezaji wa bidhaa hiyo feki. ------------------------------ |
Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii, Moshi
JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa kiwanda cha
kutengeneza Pombe "Feki" aina ya Konyagi huku likiwashikilia watu nane
waliokutwa ndani ya kiwanda hicho wakifanya shughuli ya utengenezaji
wa pombe hiyo.
Mbali na kiwanda na watuhumiwa hao pia Polisi imefanikiwa kunasa
mitambo mbalimbali iliyokuwa ikitumika kiwandani hapo zikiwemo
malighafi zilizokuwa zikitumika kufunga bidhaa hizo kabla ya kuuzwa
katika maduka ya jumla ya kuuzia Pombe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishana mwandamizi msaidizi wa polisi,Robert Boaz alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao Machi 14 mwaka huu majira ya saa 7:00 Mchana katika eneo la Kambi ya raha nje kidogo ya mji wa Bomang'ombe.
"Askari polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hawa baada ya
wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa utengezaji wa Pombe ambayo
haijaruhusiwa kisheria ikiwa na nembo ya Konyagi ndipo askari walianza
uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watu hao katika nyumba
inayomilikiwa na Elias Samson mwenye umri wa miaka 31"alisema Boaz.
Kamanda Boaz alisema watuhummiwa hao pia walikutwa na lita 400 za
pombe ikiwa imehifadhiwa katika mapipa tayari kwa ajili ya kujazwa
katika vifungashio pamoja na Katoni 46 za pombe hiyo zote zikiwa na
nembo ya Konyagi.
Mbali na vitu hivyo Boaz pia alisema watu hao walikutwa na Makasha
tupu 178 ya kuhifadhi Konyagi yakiwa na nembo ,Pipa tupu 10
zinazoaminika kuhifadhia pombe hiyo wakati wa utengenezaji na Mihuri
miwili inayoonesha tarehe ya kutengezea na taraehe ya mwisho wa
matumizi ya bidhaa .
"Katika vitu vingine tulivyo wakuta navyo ni pamoja na majiko ya
mafuta "Ya Mchina"zaidi ya matano,vifaa vingine ambavyo ni kama Pasi
vilivyokuwa vikitumika kwa ajili ya kuchomea karatasi za nailoni baada
ya kujaza hiyo Pombe"alisema Boaz.
Kamanda Boaz aliyetembelea eneo kilipokuwepo kiwanda hicho aliwataja
waliokamatwa kuwa ni pamoja na George Kisivani (28), Yusuf George
(33), Preygod Urassa (27) na Richard Leonard (35) Hagai Nelson (38),
Jackson Shayo (29), Greyson Jonathan (27) wote wakazi wa Arusha pamoja na Mohamed Rashidi (44) mkazi wa Dar es Salaam.
Makasha na vifungashio
vyakutwa na alama ya TBS na TRA.
Katika hali isiyo ya kawaida Makasha ya bidhaa hiyo Feki yamekutwa
yakiwa na alama ya Ubora itolewayo na shirika la viwango Tanzania
,(TBS) huku karatasi zenye Pombe zikiwa zimebandikwa karatasi
inayotumiwa na mamlaka ya mapato nchini (TRA).
Kamanda Boaz alisema uwepo wa alama hizo mbili ni kutaka kumuaminisha mnunuzi pamoja na mtumiaji wa bidhaa hiyo kuwa ni halali na imethibitishwa na taasisi hizo mbili muhimu zinazosimamia Ubora wa bidhaa pamoja na mapato.
Alisema uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini watengezaji wa
Makasha hayo,pamoja upatikanaji wa alama hizo za TRA huku akiongeza
kuwa mbali na kosa hilo la kutengeneza bidhaa bandia pia watu hao
wanashiriki katika kuhujumu Uchumi wa nchi.
"Huu ni uhujumu Uchumi kwa sababu wametengeneza bidhaa feki ,harafu
wanaziuza madukani bila ya kulipia kodi,wakiwaaminisha wauzaji wengine na watumiaji kuwa bidhaa yao imethibitishwa na TBS na wanalipa kodi kwa kuweka alama ya TRA"alisema Boaz.
Kutokana na hali hiyo kamanda Boaz alisema tayari amefanya mawasliano na Uongozi wa shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya mapato nchni (TRA) ili kuondoa utata uliopo hku akiongeza haja ya kutolewa kwa elimu ili kuzuia athari za matumizi ya bidhaa zisizokuwa na ubora.

Ndg.david Mugwasa Bosi wa Konyagi Halali TDL (Taznania Distileries Limited),
ReplyDeleteUmeona wazalishaji Konyagi wa Mafichoni hao?
Maisha ni akili ndugu zetu Kilimanjaro, lakini siyo kufikia kubishana na kushindana Kibiashara na Ndugu yetu David Mugwasa Mkurugenzi wa Konyagi Limited ya halali ya Dar Es Salaam ambayo Kiwanda kina Leseni halali ya Serikali,Kinatoa ajira na kinalipa Kodi!
ReplyDeleteNdugu zetu Kilimanjaro mmeachana na Siasa za Chedema tulikuwa mnaenda kwenye bishara za halali na mtajali mustakablai wa nchi yetu na maslahi yake kiuchumi na hatma ya afya za wananchi, kumbe na sasa mnahatarisha zfya nza watu na mnahujumu Uchumi kwa kufyatua Konyagi feki?
ReplyDeleteTungeomba serikali iangalie kwa makini uuzaji wa hii pombe kwenye vimifuko vya plastiki (viroba).Upatikanaji wake na bei yake vimeleta mdhara makubwa huko vijijini. Vijana wadogo wanalewa na kazi za maendeleo kama kilimo hazifanyiki tena.
ReplyDelete