Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo. Picha na Ikulu |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa
Afrika Kusini.
Ujumbe
huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana
na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.
Mara
baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu
uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi
zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa
Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo kwa
Rais Kikwete.
Imetolewa
na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16
Machi,2013
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...