Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu na naibu katibu wa Bunge Maalum la katiba katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Dodoma leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Katibu wa Bunge Maalum Mhe Yahya Khamis Hamad. Wa pili kushoto akishuhudia  ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu
 Dkt. Thomas Kashililah akila kiapo kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Wa pili kushoto akishuhudia kiapo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta,Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh.Samia Suluhu, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Sefu Iddi, Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt.Thomas Kashilila na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la katiba aliyemaliza muda wake Mh.Pandu Ameir Kificho. Picha na Freddy Maro.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. The mdudu,naiona kwambali neema inaingia ndani ya Tanzania yetu mungu ibariki Tanzania na mungu awape ugonjwa usiotiba wale wote wasioitakia mema Tanzania yetu.mm ntaipenda Tanzania hatanikiwa na njaa.ntaipenda ijapokua nipo uingereza,ntaipenda popote ntakapokua,niko tayari kwenda vitani kuipigania Tanzania,mwisho saramu kwa watanzania wote popote mlipo na muwe sarama kabisaa.

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana Mhe.Raisi Jakaya Kikwete!

    Sasa tunashukuru Filimbi umesha ipuliza tumalizie mchakato wetu!

    ReplyDelete
  3. Siku zote rais yupo vizui wanaofanya madudud wengine. Jaman. Mimi nampenda sana jk. Much respect. Sita pia ni kiongozi hodar anayejiamini na afanyacho. Si mbabaishaji.katiba yenye macho na inayoona matatizo ya watanzania hiyooo yaja. Mungu awasimamie katika hili. Amen

    ReplyDelete
  4. Ushauri wa nia njema. Tunapokuwa na hafla rasmi kama hizi, wale jamaa wanaosimama kule nyuma kwenye viwanja wakati wa kupiga picha wangeombwa kuondoka wasichafue madhari ya kumbukumbu kama hizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...