Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge
Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dododma
kesho kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado
hawajaapishwa. Hivyo Wajumbe wote ambao
hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge
Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa
2:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya
kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji
Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu
ya Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge
Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe
wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa
Kamati za Bunge Maalum na saa 10:00
jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum.
Atakayeipata taarifa hii amjulishe mwenzake.
Imetolewa
na Ofisi ya
KATIBU
WA BUNGE MAALUM
Haha, waheshimiwa wameenda kupata siesta. Do we actually need thsi Bungu. I thought Warioba covered most of the wananchi interests. What are these people actually discussing. 4 weeks now and they have done nothing.
ReplyDeleteNauliza ni nani atakayetoa semina ya Rasimu kwa Wajumbe wa Bunge maalum?
ReplyDelete