mafunzo juu  sheria ndogo ya mfuko  wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya 
Viongozi  wa Halmashauri ya Nyasa  mkoani  Ruvuma  wakiwa katika  mafunzo 
Viongozi  wa  Halmashauri ya  Nyasa mkoani Ruvuma  wakiwa  katika  picha ya  pamoja na  watumishi wa mfuko  wa Taifa wa  bima ya Afya  (CHIF) ambao  walitembelea  Halmashauri  hiyo  kutoa mafunzo juu  sheria ndogo ya mfuko  wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya


 mkuu wa mkoa wa Ruvuma  Said Mwambungu

Na  Francis Godwin Blog Nyasa ..
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit  Mwambungu  amewataka  viongozi  wa Halmashauri  ya Nyasa  mkoani humo  kuendelea  kutoa  elimu  kwa  wananchi  ili  kujiunga na mfuko   wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya  


Mkuu  huyo  wa  mkoa  alitoa  rai  hiyo  wakati  wa  warsha  ya  Viongozi  wa  Halmashauri ya  Nyasa mkoani Ruvuma    pamoja na  watumishi wa mfuko  wa Taifa wa  bima ya Afya  (CHIF) ambao  walitembelea  Halmashauri  hiyo  kutoa mafunzo juu  sheria ndogo ya mfuko  wa afya  ya  jamii (CHF) ktk Halmashauri  hiyo  mpya .

Alisema  kuwa CHF ni Mfuko wa Afya ya Jamii, ulioanzishwa kisheria kupitia Sheria Na 1 ya mwaka 2001 (SURA 409 ya Sheria za Tanzania) ili kutoa huduma za matibabu kwa jamii iliyopo katika sekta isiyo rasmi mijini na hasa vijijini katika ngazi ya halmashauri, tarafa kata na kijiji hivyo iwapo  viongozi  hao  watahamasisha  jamii kujiunga ni wazi  jamii  hiyo  itanufaika na huduma  hiyo.

Hata  hivyo  alisema  kuwa kujiunga na huduma  hiyo ni utaratibu wa hiari unaoiwezesha kaya kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima kwa kuchangia mara tu kiasi cha shilingi 5,000/= au 10,000/= kwa kadiri jamii yenyewe katika Halmashauri husika itakavyoamua hivyo ni jambo zuri  ambalo wananchi  watanufaika nalo   iwapo  watajiunga .

Mwambungu  alisema  kuwa Serikali kwa upande wake inachangia kwa kiwango ambacho kaya inachangia hivyo kuufanya Mfuko huu kujulikana pia kwa jina la Tele kwa Tele.  

"Mfuko huu ulianza kwa majaribio wilayani Igunga mwaka 1996 na baadaye kuenea katika Halmashauri mbalimbali nchini ijapokuwa kasi yake imekuwa sio ya kuridhisha. ....Mwaka 2007 Serikali iliamua kuwa Shughuli za Mfuko huu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ziwianishwe.....hatua hii ilisababisha Serikali kuu mwezi Juni 2009 kukasimu mamlaka yake kitaifa ya kusimamia na kuendesha CHF  kuwa chini ya NHIF wakati Halmashauri zikiendelea na majukumu yake ya awali"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...