Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Freddy Liundi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo juu ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bandari ya Mwambani kwa kiongozi wa timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy.
Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo, kutoka Tume ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Maduka Kessy (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya mwambani ambapo upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga akionesha eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
Picha ikionesha eneo la mwambani ambako ndipo miundombinu ya bandari itajengwa.
Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Freddy Liundi (wa pili kulia) ufukweni mwa bahari, eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
Picha na Joyce Mkinga
hivi bandari ya bagamoyo wameishajenga?? manake wengine tuko ughaibuni tunabeba box hatujui nini kinaendelea bongo. last time nilisikia ujenzi wa bandari bagamoyo pamoja na reli kuunganisha tanzania, rwanda, burundi. je mradi huo umekamilika sasa serikali inaelekeza nguvu ujenzi wa bandari ya tanga??
ReplyDelete'CoW' hii ndio itakuwa kiboko yao!
ReplyDeleteTunatakiwa tuseme kwa kutenda kwa kuwa ili kujibu mapigo dhidi ya hawa jamaa ''The Coalition of Willing'' Tanzania tunatakiwa tuzungumze na kuwajibu kwa mambo ya namna hii!
Maafisa fanyeni haraka Bandari hii ikamilike na pia ile ya Bagamoyo!
Mambo yatakayo tuweka juu ni haya hapa kama yatatekelezwa ipasavyo kama yalivyo kwenye Makabrasha:
1.Bandari hii ya Mwambani-Tanga.
2.Bandari Bagamoyo na Reli yake.
3.Bandari ya Mtwara upanuzi wake.
4.Uwanja wa ndege mpya wa Mtwara.
5.Mitambo ya Gesi Lindi na Mtwara.
6.Mitambo ya umeme Kinyerezi Dar.
7.Badnari ya Dar kuongezwa ufanisi.
Hayo mambo saba (7) hapo juu ndio yata wafanya Maraisi wa Cow ambao Miradi yao kama LAPSSET inasuasua, ndio itawafanya kuja kutoa Shikamoo zao kwa JK Magogoni!
Tanga serikali ikiikumbuka itakuwa kitovu cha uchumi.jiji liko ok saaaana na ni rahsi kuweka miundombinu BIG UP JEI KEIII .JAMAA WATATUPIGIA SALUTE.
ReplyDeleteMdau wa pili umesahau mradi mmoja mkubwa wewe.Kwa kukukumbushia ni ule mradi wa Tanganyika kuimaliza kuimeza Zanzibar au kuigoa yote..
ReplyDeleteMdau wa 4 umeula wa chuya!
ReplyDeleteWewe ukiwaza kuvunjika Muungano ndio kwanza Muungano unazidi kukomaa siku hadi siku.
WEWE TAFUTA UWEZEKANO KUHAMA KUTOKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UHAMIE OMANI.
Labda MRADI MKUBWA ULIO BAKIA hapo alivyo sema Mdau No.2 ni wewe Mdau wa 4 KUPATA PASIPOTI YA OMANI NA KUHAMIA HUKO!
Mdau wa 4 Mdau wa pili amesahahu Mradi mwingine muhimu sana!
ReplyDeleteNI MRADI ULE WA WAPINGA MUUNGANO KAMA WEWE NO.4 PAMOJA NA WENZAKO KUHAMIA ARABUNI OMANI MKALE TENDE NA MAZIWA PAMOJA NA KURUDI KWENYE MAKUCHA YA MKOLONI WA KIARABAU HUKO MASCUT-OMANI!
Fredy liundi ni kaimu manager wa bandari ya tanga? safi sana. Naona Kikwete kaamua kuwapa kazi vijana sasa. inapendeza sana na inatia moyo kuchapa kazi. wazee wapumzike tuwalee. mpeni kijana umanager kabisa sio akaimu
ReplyDelete