MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, na wadau mbalimbali wa afya leo walizungumzia madhara ya ugonjwa hatari wa homa ya ini kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana Jijini Dar. 
Miongoni mwa wadau waliokuwa kwenye mkutano huyo ni madaktari mbalimbali, Sanofa ambao huhusika na vipimo vya ugonjwa huo, Damu Salama ambao huhusika na upimaji wa damu na SD Tanzania.
Shigongo akizungumza kwa masikitiko jinsi watu wengi walivyo kwenye hatari ya kufa kwa ugonjwa wa ini.
…Akiwa na jopo la madaktari. Kushoto ni Dk. Mtebe Majigo, Mganga Mkuu wa Amana, Meshack Shing'wela (wa pili kulia) na Daktari Kiongozi Andrew Method.
Ndeonasio Towo kutoka Damu Salama akielezea umuhimu wa wananchi kupima damu kubaini maradhi mbalimbali bila kusahau virusi vya homa ya ini.
Mwakilishi kutoka SD Tanzania ambao ni wadau wa ugonjwa huo, Phillip Sawe, akielezea umuhimu wa kupima mapema ugonjwa huo kabla mwili haujashambuliwa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...