1069410_488216681262565_60269170_n
Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa EALA nchini Kenya na hicho ndicho alichokisema kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
----------------------------------
Nimerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara, wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.
Ziara hii imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi (people Centred Integration).
Kama nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia bado mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu ni kubwa.
Hata hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanashiriki kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa wabunge wa EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji.
Ni imani yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa kuwaalika wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado ufahamu wa wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni changamoto kubwa.
Lengo kuu la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa EA ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au kutokufikiwa kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Watanzania tunafahamu faida za EAC tatizo ni hao washirika wetu wanapogeuka ndumila kuwili

    ReplyDelete
  2. MsemaKweliMarch 01, 2014

    Sasa hapo mimi mbona sielewi? Huyu ni mjumbe/mbunge wa EAC na anatoka Tanzania kwanini wao wasielekeze nguvu kwa kutoa elimu kwa Watanzania ya hizo faida za EAC na kuielewe jumuiya pamoja? Kwanini hili liwe jukumu la serikali ambayo ina mambo mengine mengi ya kuyasimamia? Kama hawa wabunge wa EAC hawataweza kutoa elimu na faida ya jumuiya mpaka serikali itoe, je ni faida gani ya kuwa na hawa wabunge?

    ReplyDelete
  3. Kwani kazi za Wizara ya Afrika Mashariki ni nini?

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa nakumbuka mlitukuta tukiogelea kwenye bwawa huko Naivasha kwenye mitambo ya kuzalisha umeme. Mbona hugusii changamoto za maendeleo ulizoziona. Barabara za juu, upanuzi mkubwa wa uzalishaji umeme. Mshauri Magufuli ajenge barabara za juu. Mpaka sasa kuna ahadi ya barabara moja tu pale Tazara. Integration iwe ni pamoja kuiga maendeleo ya wengine.

    ReplyDelete
  5. angalieni umoja wa ulaya na matatizo yake ,wao bado wana uwezo kifedha , kiufundi na kwa kila hali lakini wapi maendeleo ni madogo na matatizo ni mengi, kila mtu kivyake abebe mzigo wake, hii jumuiya inatakiwa ife ili tuendelee , lakini kuna mataifa ya nje yanashinikiza kuwepo huu muungano wa EAC kwa faida zao tuwe waangalifu , kila mtu abebe nchi yake aiendeleze anavyotaka kushirikiana sana mwisho ni kugombana , vyombo vikaa pamoja haviishi kugongana na kuvunjika ,

    ReplyDelete
  6. The mdudu,nyie kama wabunge ndio kazi yenu hiyo muwe na wivu wa maendeleo kila mnapo yaona huko kwa wengine mtuletee hapa Tanzania mawazo yenu na mikakati yetu ni muhimu kwa taifa letu la Tanzania,,sasa ww kama mbunge tayari ushajitoa na unaisukumizia serikali,sisi watanzania tunataka na nyie mchakali hiyo ndio kazi tuliokutumeni msituletee mchezo hapa wakati nyie mnaingiza MAMILIONI YA PESA HUKO,mjiulize wenyewe kwanza wabunge wa kutoka Tanzania hivi kwanini KENYA imeweza kujenga barabara za juu? Kwa nini sisi tusiweze? Hayo ndio mambo yenye umuhimu ya kujiuliza? Hatutaki mambo ya kulala huko bungeni,hii ni aibu kubwa nanimatusi makubwa kwetu Kanchi kadogo kama kenya kisha katuzidi kiuchumi.amkeni watanzania kwenye usingizi mzito na muwe wazalendo na nchi yenu na kila mtanzania ajitume na kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuichukia RUSHWA huo ndio mwarobaini wa maendeleo amka amka mtanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...