Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Uzalishaji Mali  la Jeshi la Kujenga Taifa,  SUMA JKT, limepongezwa kwa juhudi zake katika kuhakikisha ulinzi unaimarika katika maeneo ya mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo Kagera.

Mgodi huo kwa sasa umekabidhiwa kwa serikali ambapo unaendeshwa chini ya shirika la madini la STAMICO.

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa STAMICO,  Rumisha Kimambo katika kikao kilichojumuisha Bodi yake na uongozi wa mgodi wa huo kilichofanyika mgodini hapo  hivi karibuni.

Mwenyekiti huyo ambae pia alipata fursa ya kutembelea eneo la westzone na mojamoja uliopo Mgodi huo alionesha kuridhishwa na mfumo wa mbinu shirikishi zinazotumiwa na mgodi huo katika kulinda mgodi bila ya kuharibu uhusiano kati ya mgodi huo na wananchi.

“Tumefurahishwa sana na kazi inayofanywa na SUMA JKT hapa STAMIGOLD kwani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana  kuondoa tatizo la wachimbaji haramu na wavamizi ndani ya  mgodi.” 

Alisema kuwa wachimbaji haramu wengi katika migodi ni tatizo na kunakuwa na njia mbadala katika kuwakabili kitu ambacho SUMA JKT imefanikiwa.

Shughuli za uchimbaji katika mgodi huo zinatarajiwa kuanza  mwezi April mwaka huu baada ya kukamilika kwa barabara ya urefu wa takribani Kilometa 3.9 kutoka eneo la ofisi za Mgodi kuelekea kwenye maeneo ya uchimbaji.

Mapema mwezi huu kampuni ya African Barrick Gold  iliyokuwa ikimiliki mgodi wa TULAWAKA ilifanikiwa kuhamisha  kibali  na baadhi ya leseni  za uchimbaji  katika eneo la westzone na mojamoja kwa shirika la madini STAMICO hivyo kuwezesha shirika hilo kuwa katika nafasi nzuri ya kuendeleza sekta ya madini hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...