Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) anasikitika kutangaza kifo cha Mfanyakazi wa Wakala Mhandisi Charles M. Madinda kilichotokea ghafla leo jumamosi tarehe 8/3/2014 katika hospitali ya Amana – Ilala Dar es Salaam. Habari ziwafikie Wafanyakazi wote wa TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake zote pamoja na ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Morogoro siku ya Jumanne tarehe 11/3/2014. Marehemu ataagwa kesho Jumapili saa tano asubuhi kwenye hospitali ya Amana – Ilala Dar es Salaam. Tunatoa pole zetu za dhati kwa watoto wa marehemu, ndugu, majirani na marafiki.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. 
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...