Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel akifungua Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 : Mgeni rasmi katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akitoa hotuba fupi wakati wa tamasha hilo, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel.
 }: Mshereheshaji kutoka kikundi cha Temeke akionyesha umahiri wake kwa kula moto wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi lililofanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa makundi ya muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi kipya na Utenzi waliooshiriki katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi wakiwa katika picha ya pamoja ambapo katika mziki wa dansi kundi la Msondo ngoma liliibuka kidedea huku upande wa taharabu Jahazi Modern Taharabu walishika nafasi ya kwanza huku muziki wa kizazi kipya msanii Kelvini Nyoni kuwabwaga wenzake na katika fani ya Utenzi Bi. Mariam Mponda kushika nafasi ya kwanza.
 Kundi la muziki wa dansi lijulikanalo kwa jina la Mashujaa wakitumbuiza wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ha ha ha taharabu?!!!! asante Michuzi kwa kunichekesha sana.

    ReplyDelete
  2. Taharabu ndiyo nini Ankali,?

    Maelezo '' Muziki wa dansi, Taharabu, kizazi kipya na utenzi'' nukuu toka habari iliyoletwa na WHVUM !

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...