Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimweleza Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon, Mipango mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea Ikiwamo ufunguaji wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea, wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimweleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda mpango wa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala yatakayochangia maendeleo kwa nchi na wananchi husika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati za Mambo ya Nje za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Korea ipi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inazungumziwa korea ya kusini( 태한민국)

      Delete
  2. korea kusini. EL anatisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...