Semina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba leo imelazimika kuahairishwa baada ya kuibuka vurugu ndani ya ukumbi wa Bunge. 
Zogo hilo liliumuka baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya wajumbe uliosababishwa na kutuhumiana kwamba zipo dalili za upendeleo wanazofanyiwa baadhi ya wajumbe kutokana na sababu za kiitikadi za vyama. 
Hali hewa ilichafuka  baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya Mjumbe Mhe. Christopher Ole Sendeka ambaye aliingia katika mvutano na Mjumbe wa Kamati ya Kanuni Mhe Abubakar Hamis Bakari kuhusiana na uwasilishwaji wa majedwali ya marekebisho ya kanuni. 
 Awali Mhe. Sendeka alipewa ruksa na Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo Mhe Pandu Ameir Kificho,  awasilishe mapendekezo ya mabadiriko katika kifungu cha 58 cha kanuni hizo kilichokuwa kikijadiliwa muda huo. 
 Lakini baada ya Mhe.  Sendeka kuwasilisha mabadiliko yake, alisimama Mjumbe Bakari ambaye kiutaratibu alipaswa kujibu hoja hiyo hasa kwa kuwa ni mjumbe wa kamati ya kanuni. 
Mhe. Bakari alikataa kupokea hoja ya mabadiliko ya Mhe. Sendeka kwa kusema kuwa hayakuwa yamewasilishwa kwa kufuata taratibu za uwasilishwaji wa mabadiriko ya majedwali, na kwamba Kamati haina mapendekezo hayo, hivyo haiwezi kujibu jambo lisilo jadiliwa. 
Katika kukataa huko Bakari alikitupia lawama kiti cha Mwenyekiti huyo kwa madai kuwa kimekuwa kikitaja majina ya wajumbe na kuwapa nafasi ya kuongea wakati hawapo kwenye utaratibu wala hawakuwa wameomba toka awali. 
 Aliongeza kuwa si kwa Mhe. Ole Sendeka pekee, bali pia Mwenyekiti huyo amekuwa akiataja wajumbe wengine wakiwamo Peter Serukamba pamoja na Umy Mwaimu ambao wote hawakuwa wamewasilisha majedwali ya mapendekezo ya marekebisho toka awali. 
 "Mheshimiwa Mwenyekiti, Ole Sendeka hayupo katika orodha ya walioleta mapendekezo, lakini nashangaa wewe unampa nafasi ya kuzungumza wakati hakuwapo kwenye orodha yetu, kamati hatuwezi kumpa nafasi ya kujibu hoja yake hatuitambui. 
"Hata hao wakina Ummy Mwalimu hawapo katika orodha. Mwenyekiti ukiendeleza huu mtindo wa kuruhusu kila anayetaka kuzungumza hapa azungumze hatutofika. tutatumia miezi 6 hapa kutengeza kanuni tu. Lazima uwe na maamuzi kuwa wanaoleta mapendekezo hivi sasa hatupokei"alisema Mhe Bakari 
 Baada ya Mhe Bakari kumaliza kuzungumza, Mhe Kificho aliingilia kati na kusema kuwa jambo hio linaweza kuwa limechanganywa na sekretarieti inayoandaa na kwamba yeye binafsi amepewa majina ya waliopeleka marekebisho hivyo anashangaa kuona kama hayapo kwa wajumbe hao. 
Mhe Kificho alitoa ruksa kwa Mhe. Ole Sendeka kuongea tena, ambapo katika mazungumzo yake alisema kuwa mapendekezo yake aliyawasilisha mapema na kwamba kama Mhe Bakari ana itikadi zake za vyama hivyo asimuhusishe humo. 
 Mhe. Ole Sendeka alisema kuwa yeye ana uzoefu wa kanuni na kwamba alifuata taratibu akiwa na wenzake - Mhe Serukamba pamoja na Mhe Mwalimu - na kwamba kama mapigo yao yanawaumiza wajumbe wengine wavumilie tu. 
 "Mheshimiwa mwenyekiti tuliopo hapa ni wajumbe. Nilijua na mimi sio dhaifu kwenye kanuni. Nnaijua haki yangu kwa kuwasilisha kwa wakati, nilitimiza wajibu wangu, kama mapigo yetu yanawaumiza. 
 "Kazi yetu si kupeleka majina yetu kwa Abubakari. Kama yeye ana chama chake na hoja zetu zinamuuma, asimame na kutuweka wazi kuwa yupo katika msimamo gani. Lakini mimi nimewasilisha kama taratibu zinavyonitaka"alisema Ole Sendeka 
 Kauli ya Mhe Sendeka ilianzisha sintofahamu ndani ya Bunge hilo baada ya baadhi ya wajumbe kuanza kuzomea na wengine wakisiama na kutaka kupewa ruksa ya kuzungumza huku wakiwasha vipaza sauti.
 Hali hiyo ilimuinua Mhe Kificho kitini pake ambapo  aliwasihi wajumbe kuacha kuingiza masuala ya vyama hasa kwa kuwa wajumbe walioingia hapo ndani wamewakilisha makundi. 
"Niwaombe wajumbe tujitahidi sana, tusionyeshe misimamo ya vyama, tumepata heshima kubwa ya kuwapo humu ndani hivyo si vyema kuanza kuonesha vidole kwasababu huyu katika CCM, sijui CUF ama Chadema au kokote itaibua hisia ambazo si vyema.
 "Mheshimiwa Ole Sendeka naona ulimi umekwenda mbali kidogo... ukamgusa mheshimiwa Bakari. Mimi naona hili jambo limekwenda nje. Kwa hiyo naomba tuwe makini"alisema Kificho.
  Baada ya kauli ya Kificho, wajumbe walianza kupiga kelele wakitaka Mhe.  Ole Sendeka kumwomba radhi Mjumbe Bakari, huku wengine wakimtaka asifanye hivyo. 
Mhe Kificho alitoa nafasi nyingine kwa Mhe Bakari kuzungumza, ambapo katika mazungumzo yake ndipo hali ya hewa ikachafuka. 
 Mhe Bakari alisema kuwa alichosema yeye ni kwa faida ya Bunge na nchi, na kwamba taratibu ni kuwasilisha mapema mapendekezo na kwamba majina ya kina Sendeka hayakuwapo. 
 "Mimi nilizungumza vizuri hili kuweka utaratibu mzuri wa kupokea majedwali haya. Mheshimiwa mwenyeiti kwa bahati mbaya mdogo wangu Ole Sendeka anadai kanuni anazijua vizuri....Lakini ninachosema sifikirii..sifikirii kama ana uzoefu wa kujua kanuni kunishinda mimi.
"Mheshimiwa mwenyekiti toka mwaka 1980 nipo katika mabunge haya! Kwa hivyo sifikirii kama mtu katoka Simanjiro miaka 10 iliyopita anaweza akaja hapa na kusema anajua kanuni kunizidi. 
 "Mimi sitaki aniombe radhi. Ila ninachotaka kumfahamisha ni kwamba kuna watu wana ujuzi zaidi kuliko yeye!!! Hivyo awe makini katika mazungumzo yake...,"alisema Bakari 
Kauli hiyo ilizidisha mgawanyiko katika Bunge hilo, ambapo wajumbe walisimama na kuanza kupiga meza wengine wakizomea.  
Baadhi ya wajumbe walionekana wakirushiana maneno na hata  kutaka kurushiana makonde. 
Askari ambao ni wapambe wa Bunge ilibidi kusogea karibu ili  kutuliza vurugu hizo, huku wajumbe hao wakiendelea kurushiana maneno. 
 Vurugu hizo zilionekana kusambaa katika ukumbi mzima kwa wajumbe  kurushiana maneno makali. Ndipo Mhe Kificho akaamua kuahirisha Semina hiyo.

Sehemu ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakitawanyika mara baada ya mwenyekiti kuahirisha kikao kutokana na baadhi ya wajumbe kutoelewana katika hoja.Semina imeahirishwa hadi saa 11.00 jioni.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ole Sendeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tuhuma za baadhi ya wajumbe kuwa Mwenyekiti anampendelea kwa kumpa nafasi nyingi za kuchangia hoja katika semina ya kanuni za bunge maalum.
Mjumbe wa Bunge la Katiba na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Mhe. Freeman Mbowe akiongea na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo,mara baada ya kuahirishwa kwa kikao.
Mjumbe wa Bunge la Katiba,Mhe. Kajubi Mkajanga kutoka taasisi ya vyombo vya Habari akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mwemyekiti kulazimika kiuahirisha semina ya kujadili kanuni hadi saa kumi na moja (11:00) jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ankali,
    Tundika Video ndefu kuhusu yaliyojiri ktk vikao vya kila siku maana haya mambo ya 'ukodaki' bila maelezo kupitia video ktk karne hii, wakti huu, muda huu hutufanya kukosa mengi.

    ReplyDelete
  2. Hii hali ya hewa inachafuka chafukaje mapema hivi jamani?. Mjue sisi wananchi tunawaangalia nyinyi kwa mategemeo makubwa ya mchango wenu.

    ReplyDelete

  3. Hii hali inanikumbusha wakati ule wa kuijadili katiba ya uhuru wa Zanzibar mwaka 1963 pale Lancaster House,London ambapo wajumbe wa ASP wakati ule walisusia kikao kwa nusu saa hivi.Kwa hali hii nawasihi watanzania wenzangu kuwa msitaharuki maana mambo yana watu wenye mvi na mahekima yamewajaa pomoni vichwani. Situation is not critical and it is under control.

    ReplyDelete
  4. Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kwanini huwa tunajikongoja kila mahala, Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa Bunge hili la katiba utaelewa kwamba tatizo la uzembe, uvivu, ubishi, ulimbukeni, ujuaji na mengineyo ni matatizo ya Kitaifa na si watu binafsi. Ni wiki kadhaa sasa zimepita na hakuna lolote lililofanyika katiaka uundwaji huu wa katiba mpya.

    ReplyDelete
  5. Pendekezo: Wabunge wakiahirisha bunge wasilipwe posho ya aina yoyote kwa hizo siku za ziada! Huenda kwa kufanya hivi watakuwa na nidhamu na kukubaliana kwa wasiyokubaliana.

    ReplyDelete
  6. It is highly profilic and positive whenever we have time and opportunity to file a comment on this blog.

    As I have always put out to your readers, I am a "migrant" worker in Kenya from where my work takes me all over places which would interest only a few of your readers.

    I find lots of pleasure whenever i am back to drop a line on my experiences to help me compare my home experience with the diaspora.

    I am just back from Somaliland where i tried to entice the port of Berbera join the insititution I work for. But my institution is for soverign countries, and Somaliland is not yet recognized as such.

    It was during this visit that the performing arts big news hit Kenya with Lupita Nyong'os Oscar gong. I was pleased like my Kenya colleagues and the film and theatre world as such, recalling my own brief stints in films in Tokyo with Martin Mhando exactly thirty years back. We knew little or nothing about Oscars then and our dreams were not even valid as young University dramatists then.

    Anyway Lupita has made. The Oscar this week is not trending as is about her looks, very natural luoish including the Prada dress or her Clarin lip gloss which is available on line only since she dropped one into a fund raiser hat on March 2.

    I think seriously about the performing arts back home and is left to wonder whether in another 70 years we will produce a nominee for the Oscars. Bongo movies. Produced from almost no budget at all because most of the facilities are makeshift, borrowed, that is they go to plushy homes and ask the owners to let them ati Kufanya shooting or the sham skills they have and we keep on praising.

    Yet it is not Lupita whom I want to caomment aboaut here. Rather it is about the Exam results for the Secondary Schools that were released here last week.

    I was driving down one of the streets where the law courts are in Mombasa when I came head on with a huge procession of peaceful young chaps waliovalia hizo school uniformss.

    Na there were cars in the procession and malights zikiwa on kama vile ni football club imewin Champions league. Seriously.

    Waving from the moon window were some adults as well. Sasa I thought someone has overturned an election victory. Hakuna. It was about Aga Khan Secondary School emerging top of the coast county in the exam. Every body was so ecstatic, hata pedestrians.

    So this took me back home. When do we reaaly have such euphoria over exams. hata hiyo NECTA ikitangaza, it is just the family which produces the best student that celebrates with the mdeia giving them a filler space. Hapa Standard and Nation ran front page and inside pages stories for almost the whole week, only until ODM shambled elections and the current debate on whether regional commissioners should be called Waheshimiwa and fly national flags heated up, did the schools fall grade to middle pages.

    Do we, if I may ask, as a broad academic society condone school performance competitiveness or just focus on one family child.

    It is time more pages and more objective reporting on these achievements were available.

    ReplyDelete
  7. Ndiyo. Video tafadhali Michuzi. Tujue kasemaje Mwandosya, kasemaje Mbatia na wajumbe wamepokeaje.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...