Gari likiwa limebeba matenga ya nyanya kutoka shambani,katika kijiji cha Magubike,Iringa Vijijini mapema leo,tayari kwa kusafirishwa kupelekwa mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuuzwa,Mmoja wa wakulima wa zao hilo la Nyanya aliyejitambulisha kwa jina moja la Ezekiel alieleza kuwa wakulima wengi wa zao hilo kwa sasa wako kwenye mavuno,akaongeza kuwa changamoto kubwa walionayo ni suala la barabara kwa ajili ya kusafirisha mazao yao,si ya za uhakika sana kutokana na jinsi zilivyo,"hapa mvua ikinyesha tu ni shida sehemu kubwa ya barabara magari yanashindwa kupita kwa sasa miundombinu yenyewe ni mibovu,hivyo tunaiomba serikali iangalie pia suala la miundombinu kwa wananchi wa kijiji hiki,angalau basi barabara iwe ya uhakika na inapitika.ili mazao yetu yasituharibikie/ozea nyumbani ama mashambani" alisema Ezekiel.
Home
Unlabelled
TUNASHINDWA KUSAFIRISHA MAZAO YETU KWA SABABU MIUNDOMBINU SI YA UHAKIKA-MKAZI WA MAGUBIKE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bwana Ezekiel, pole kwa ukulima.
ReplyDeleteNi aibu sana mazao yenu yakioza nyumbani au kwenye mashamba kwa ukosefu ya usafiri wa mazao.Another solution is to ask for construction of a tomato processing plant to produce market stable products such as Tomato ketchup, tomato puree and sauce and paste,tomato juice and canned tomatoes, hapo hapo kwenu.Jee mmewahi kutafuta ujuzi wa kutengeneza sun-dried tomatoes?