Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Kipya cha Televisheni (TV 1 Tanzania),Marcus Adolfsson akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Southen Sun,jijini Dar es Salaam leo,wakati wa kutangaza Uzinduzi wa Kituo hicho cha Televisheni kitakachokuwa kikirusha matangazo yake kutokea Jijini Dar na kuonekana nchi nzima.
Watangazaji wa Kipindi cha The One Show kinachorusha na Kituo hicho kipya cha Televisheni(TV 1 Tanzania),Jokate Mwegelo na Ezden Jumanne wakizungumzia namna walivyojipanga kwenye kipindi chao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Kipya cha Televisheni (TV 1 Tanzania),Marcus Adolfsson (wa tatu kulia) pamoja na baadhi ya watangazaji wa televisheni hiyo.toka kulia ni Ezden Jumanne,Jokate Mwegelo,Meshack Nzoha na Agness Kahonga,wakiangalia moja ya vipindi vyao wakati wa uzinduzi huo.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
TV 1 Tanzania, Msisahau wana Diaspora ughaibuni kwa kuonesha vipindi vyenu ONLINE na Clips ktk YOUTUBE.
ReplyDeleteMaana vituo vikubwa vingine vya TV Tanzania hawarushi matangazo ya ktk eneo la ONLINE na wala hawatundiki clips za matangazo yao ktk YOUTUBE.
Mdau
Tanzania Diaspora