Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.

Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo. 
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao. 
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhidi ya kutumia uwanja huo. 
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu.

Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. TFF mnatutania kabisa, yaani badala ya kuweka ulinzi na kutoa adhabu kwa wanaofanya hivyo mnaleta kelele sizoeleweka hapa. Wacheni utani. Siwaelewi kabisa. Ndiyo maana hatuendelei kabisa kimchezo, uzalendo sifuli. Wacheni kelele fanya kazi, piga faini watu waharibifu au weka ndani utaona wanavyobadilika. Sasa wahalifu wanawaona nyie TFF goi goi ndiyo maana wanarudia maovu yale yale. Mmeniuzi na hii habari yenu leo. Ngoja mie nije niwe mkuu wa hiyo TFF, tutanyoka tu, hata ikibidi nisimame pekee yangu, nitasimama kama Sokoine.Hamna rushwa wala siogopi uchawi wala nini. Tungekuwa mbali kweli sasa hivi.

    ReplyDelete
  2. Ndugu uliyeandika hapo juu hizo ni stori za ABUNUASI!!!! Hahahahaa....umenichekesha sana KING MAJUZI!!

    ReplyDelete
  3. Wanaofanya uhuni wa kuharibu mali za uwanja waadhibiwe kabisa au kuzuiliwa kuingia, picha zao ziwekwe kwenye milango ili wapigwe marufuku kutumia uwanja huu.

    ReplyDelete
  4. hilo la serikali kuchukua mapato yote litakua fundisho zuri

    kama kawa TFF wataonea klabu tu wakati wao hawahusiki kuandaa mechi wala kulipia hao washabiki

    udhibiti unawezekana sema kwa ujanja ujanja wa mapato wa TFF ni ndoto hilo kutokea!

    ReplyDelete
  5. mharibifu siku zote anatakiwa kuchukuliwa hatua aeleze kwanini anaharibu mali ya umma hana ,hahitaji kuhurumiwa eti jukwaa letu hatakiwi kukaa flani ivi kweli TFF NA SERIKALI KWA UMLA hawa watu mpaka wanago'a viti hivyo mlikuwa hamuwaoni? huu uwanja walioharibu mkawatangazia kuwa wamefungwa miaka 10 kabsaa huo uwanja utakuwa salama ,hatuwezi kuishi kama nchi haina sheria ,watu waishi kwa mipaka bana,watu hata sheria ndogo za utii wanashindwa!! halafu unasema eti bangi,akiadhibiwa atavuta kwa ustarabu!! juu ya hili serikali lisijirudie TFF hawawezi tunzeni mali hiyo jamani ili tungalie na viu vingine vya kufanya .muda unakwenda na umasikini unaongezeka.

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi hawa ndugu zangu wa Yanga walipe tu inasikitisha sana. Sijui huu uswahili utaisha lini...!!??

    ReplyDelete
  7. Hawa watu wanaonekana kwenye picha watafutwe waadhibiwe. Klabu zao zipewe adhabu kama Uingereza. Hakuna mchezo hapa. Hatuendelei kwa sababu ya upuuzi kama huu. Adhabu adhabu tu. Hakuna kucheka na mtu hapa.

    ReplyDelete
  8. I Can see there are lots to learn, if we calculate how much have been spent as a payback for destroyed chair and amenities is quite a lot. that i t could worth installing modern security system which could enable catching culprits and punish them accordingly, kifo cha wengi harusi thats why haya mambo yanajirudia maana hamna mtu ameadhibiwa solely kwa kosa hilo. kama inakuwa ngumu basi wa subcontract security system uwanjani.
    ukweli ni kuwa wale wanaofanya yale madudu uwanjani ni wabaya hata mitaani kwao. hivyo wakikamatwa na kuadhibiwa kitaifa italeta amani hata huko mitaani

    ReplyDelete
  9. Hivi hatujawa na teknolojia ya hizi picha mgando ya kuwatambua hao wanaoonekana "live"waking'oa viti?Nakubaliana na mdau,tuanze na hao wanaoonekana kwenye hizo picha,wapelekwe kwenye mkono wa sheria kali.

    David V

    ReplyDelete
  10. Mdau #2, ni kweli tunacheka kama stori za ABUNUASI, lakini inauma sana aisee. Tunajaribu sana kupiga kaatua halafu watu wanaturidisha nyuma hatua millioni. Naomba ili lisiwe tatizo la timu fulani, tunaitaji Ulinzi wa kueleweka. Ukifanya vurugu lazima ujue matoke yake. Miaka miwili iliyopita nilikuwepo taifa na wageni kama 20 tunaangalia kombe la Kagame. Nilienda chooni, yaani mabomba yote yamevunjwa, na watu wanajisaidia kwenye masinki. Yaani mpaka leo siamini siye kama binadamu tunaweza kufanya vitu kama vile, au sasa kuvunja viti. Ni zaidi ya aibu, halafu TFF wanasema nini?! Na watu wapo wazi mpaka wengine wamepigwa picha magazetini, mitandaoni .n.k Unaanza kutoa hukumu kwa hao, na kama wana uwezo wa kulipa watafutie adhabu nyingine. Kama vipi, ichezeshwe mechi moja kubwa bila mashabiki, mala moja tu, wakuu wa TFF wakiona hawajapata zile pesa za pembeni watashulighulikia ili tatizo. Na uhakika kabisa ili swala likisimamiwa vizuri na uongozi(Rais Malinzi na wenzio) wanainchi watafuata. Naomba Mungu tumpate mjasili mmoja tu atakayefanya kitu sahihi.

    ReplyDelete
  11. Hapa Polisi wapate maelekezo ya jinsi ya kutumia KAMERA za photograph na VIDEO HD zenye ZOOM kali kurekodi sura za watazamaji waendekezao fujo na uharibifu na kuwachukulia hatua za kisheria na pia kuzuiwa kuingia uwanjani.

    Picha hizo zikuzwe na kutundikwa milangoni hapo uwanja wa Taifa na siku wakija tena uwanjani wakamatwe kama waliweza kuponyoka mkono wa sheria.
    Mdau
    Uwanja wa Etihad, Man City

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...