Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR) iliyo na makao yake makuu mjini Arusha leo imetoa msaada wa magari mawili ya kiusalama (Amoured Cars) kwa jeshi la polisi mkoani Arusha ili kuimarisha shughuli zake za kiusalama mkoani hapo.
Magari hayo ni baadhi ya yale yaliyokuwa yakitumika kwa shughuli za usalama kubebea watuhumiwa au watu nyeti,na mahakama hiyo inatarajiwa kumaliza shughuli zake mwakani.
Magari hayo ni yale yaliyoimarishwa kiusalama ambapo hata risasi haziwezi kupenya kwenye bodi yake au kwenye kioo chake.
Magari hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama hiyo Bw. Robert Foot kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Lebratus Sbas.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR), Bw. Robert Foot akikabidhi funguo za magari hayo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Lebratus Sabas.
Kamanda Sabas akitoa shukrani zake kwa uongozi wa UN-ICTR kwa msaada huo. Katikati ni Afisa Habari wa Mahakama hiyo Bw. Danford Mpumilwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...