Kufuatia hatua ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kuunda kamati ya muda (Tanzania UK Diaspora Task Force) itakayosimamia maandalizi ya Mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014, tunapenda kuwasilisha majina ya wajumbe wa kamati hiyo kwa Watanzania waishio Uingereza.

Kamati hiyo itakuwa chini ya Uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga akisaidiwa na Bw. Cleopa John katika nafasi ya Katibu. Aidha Bi Maxine Brown atashughulikia mawasiliano kati ya kamati na watanzania waishio nchini Uingereza.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni wafuatao:

Salim Amar: Makamu Mwenyekiti
Mariam Mungula: Makamu Katibu
Hassan Mussa: Mratibu wa Wajumbe wa Kamati
Mchungaji Mathew Jutta: Mjumbe
Kassim Kalinga: Mjumbe
Amos Msanjila: Mjumbe
Allen Kuzilwa: Mjumbe
Sheikh Rashid Saleh: Mjumbe

Watanzania waishio Uingereza mnaombwa kuunga mkono uongozi wa kamati hii katika kufanikisha mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014.

Kwa kuanzia Watanzania mnaweza kutuma maoni kuhusu mnayotarajia kuyaona kwenye Mkutano wa Diaspora mwaka 2014 kwa kujaza fomu ya utafiti iliyopo kwenye anuani ifuatayo : https://www.surveymonkey.com/s/5VVGK9Z

Aidha mawasiliano na Kamati yanaweza kufanyika kupitia mitandao ya kijamii ifuatayo: Facebook: www.facebook.com/tanzaniauk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Talaka rejea ni kwenye Ndoa tu, lakini sio kwenye suala la Uraia!

    Wewe ulishadai Talaka (Kuukana Uraia) ukapewa kwa kupata Sheria huko uliko.

    Na sasa unataka Taraka Rejea!

    NIMESHAPATA MKE MWINGINE KIJANA TENA TAJIRI SAANA ANA MALI NYING SANA ANA GESI, ANA URANIUM ANA MAFUTA NA RASILIMALI LUKUKI (MKE HUYO NI TANZANIA YA SASA TOFAUTI NA SIKU ZILE KITAMBO ULIPO KIMBIA WEWE KWENDA MAJUU).

    MUME (BUNGE LA KATIBA) NAKATAA SITOI TALAKA REJEA!

    ReplyDelete
  2. Madiaspora ninyi ni watu wa kutapa tapa sana na dunia.

    Mmeondoka TZ mkidai kuna shida mkaenda Majuu na wengine Mkadai Sheria kwa kutumia Mawakili na wengine kujilipua Ukimbizi, na wengine mkaachilia tu kizembe hadi mkapoteza Uraia kama mnavyodai.

    Na sasa mnataka na Sheria za Uraia huku mliko dai kuna shida ndio tuwaeleweje?

    ReplyDelete
  3. Si ndio ninyi siku zile kitambo mlichana Passport za Bongo baada ya kuwasili Uwanja wa ndege Heathrow Uingereza?

    ReplyDelete
  4. Pana mambo ya kufanyia masihara na Mzaha katika maisha ya mwanaadamu lakini siyo moja ya haya hapa chini matatu (3):

    1.KUPANDA JUU YA MTI NA PANGA KALI SANA AMA SHOKA KALI SANA, HALAFU KUKAA MWISHO WA TAWI LA MTI LINAKOISHIA NA KUKATA LINAKOTOKEA!

    2.KUINGIA MSALANI UKAFIKA HADI SHIMO LA MAJI TAKA, HALAFU UKATOA SARAFU YA DHAHABU YA MUUNGANO WA TANZANIA WA MIAKA 50 YENYE THAMANI YA TSHS. 50,000 HALAFU UKAANZA KUIRUSHA JUU NA KUIBWAGA KATIBU NA SHIMO LA CHOO!

    3.KUBWA LA YOTE AMBALO NI BALAA KUBWA SANA NI UKIWA NA AKILI ZAKO TIMAMU NA BILA KULAZIMISHWA KUUPOTEZA AMA KUUKANA URAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

    ReplyDelete
  5. Baada ya kupata Sheria Home Office mliona mmemaliza kilakitu katika maisha!

    Kumbe asalaleee ngoma mbichi mwaka 2014 mnakuja kukabilaiana na Wabunge tata wa Bunge la Katiba Tanzania!

    Ni afadhali mshike mshike mlioupata mlipokuwa Home Office mkifuatilia na mkidai Sheria huko UK!

    ReplyDelete
  6. Jee wale waliobadilisha majina yao asilia na kujipaka majina ya kisomali na kupewa paspoti za Uk jee kama mkirudi kuja kudai uraia pacha mpewe kwa majina gani.kama ukipwa la huku na la huko jee kwani wewe gaidi au mfanyabiashara ya maunga. Na jee kama TZ ikikupa likitokea ovu Tanzania itakuwa na nafasi gani katika macho ya kimataifa. In short guys,there is no room for u diasporant to be filled in the Tanzania citizenship database,what is left is only for new born children who are really Tanzanians,sori!

    ReplyDelete
  7. Kweli kuna wakati watu nawashangaa wanaandika kama hawana akili timamu, kweli mtu unakaa kwenye mtandao unaandika mambo ya uongo na uchochezi na unajiona huko kamili kichwani!! Mdau #1-5 na ukiona watu wako kimya hawajakujibu wanakuona wewe chizi.
    Tafuteni cha kufanya, cha kuwaletea faida. Kujifanya mnajua vitu wakati hamjui ndiyo tunaita ujinga. Ni wajinga kupita maelezo na ndiyo maana hamna mtu aliyetoa maoni wala kuwajibu kasolo mie na mie naonekana mchizi kama nyie.
    Mmbongo Chiberia.(Michuzi usibanie maana umewaachia hao waandike waliyoandika hapo juu)

    ReplyDelete
  8. Ninyi wabongo ambao mna roho za korosho mnatia aibu, siyo sote tulipo mamtoni tumeukana uraia wa bongo, nina zaidi ya miaka 20 mamtoni na bado na ganda la bongo, huku nina haki ya kuishi daima, mimi niliamua hivi toka nimefika huku, it suites me big time.
    Lakini kwa wale walioukana urai SO WHAT, wana haki kabisa ya kupigania dual citizenship, actually nawaunga mkono 100%.
    Mimi sijachukua uraia wa mamtoni kwa sababu sikutaka niupoteze uraia wa bongo.
    lakini ukweli ni kwamba kuna watanzania wengi tu wenye raia zidi ya moja na wanasepa kama kawa.
    I will be the 1st one to take uraia wa mamtoni once the law changes.

    ReplyDelete
  9. Jamani mtoto kwa mama hakui, hata kama alikosa kwa mama anapokelewa. Tutulie na tujiulize kwa nini wenzetu wanataka kurudi nyumbani? Tanzania ni nchi yao hata kama waliikana si kwa makusudi ila ni kwa sababu ya maisha. Tusiwe wahukumu zaidi bali Mungu ndiye atakayehukumu hilo. Mungu awasaidie kwa lile mnalotaka la kuwa na uraia pacha. Karibuni nyumbani.

    ReplyDelete
  10. Msipoteze muda wenu,

    Pasipoti ya Pili kutoka TZ ng'o hamtaipata! labda mkaombe Kenya, Rwanda na Uganda walikokubali huo Ututusa wa Dual Citizenship.

    Kumbukeni hapa ni JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZAANIA!

    Ohooo mtajikuta mnavuna mawe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...