WAKATI siku zikikaribia kuelekea kwenye Tamasha la Pasaka katika zoezi la upigaji kura kuchagua waimbaji, mikoa na mgeni rasmi katika tamasha hilo, waimbaji kadhaa wamechomoza kwenye mchakato wa kutoa huduma ya uimbaji katika tamasha hilo.
Kwa mujibu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama waimbaji hao wamepata nafasi hiyo kupitia mfumo wa upigaji kura kupitia ujumbe mfupi wa maandishi ya simu za mkononi.
Msama aliwataja waimbaji hao kuwa ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Voice Acapela na Sarah Kiarie kutoka Kenya. Aidha Msama alisema taratibu za upigaji kura kuelekea tamasha hilo zinaendelea, hivyo alitoa wito kwa mashabiki kuendelea kupiga kura kuchagua maeneo hayo matatu yatakayofanikisha tamasha hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...