Na Mwandishi Maalum 
 Wajumbe wanaoiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa na Mkutano wa wazi wa Tisa wa Kikosi Kazi kuhusu mapendekezo ya ajenda za malengo mpya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs), wamendelea kutetea maslahi ya Tanzania kwa kushiriki na kuchangia majadiliano ya mada mbalimbali zinazohusiana na mikutano hiyo. 
 Akichangia katika mada iliyohusu Technolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ambayo ilikuwa kati ya Mada kumi na moja, zilizojadiliwa katika siku ya pili ya Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema, Tanzania na Afrika kwa ujumla mwaka hadi mwaka imeendelea kupiga hatua katika eneo hilo licha ya changamoto mbalimbali. 
Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kutokuwapo kwa uratibu kati ya wazalishaji wa takwimu za ICT na watumiaji na kati ya wazalishaji na watoaji wa data ambao ni chanzo muhimu cha taarifa. Na kwa sababu hiyo anasema, tatizo hili kama halitarekebishwa linaweza kusababisha uchapishaji usio sahihi wa takwimu kuhusu ICT , jambo ambalo linaweza kupelekea utoaji wa maamuzi ya kisera wenye makosa. 
“Uboreshaji na Uratibu kati ya wazalishaji, wauzaji na watumiaji wa takwimu, utaepusha kujirudia kwa makosa yakiwamo ya matumizi ya raslimali fedha na watu, raslimali ambazo ni haba katika Afrika", alisema Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ndiye aliyewasilisha hoja za Afrika katika mada hiyo ya ICT. 
Aidha akasema kipengele cha takwimu za ICT kinapashwa kuingiza katika mikakati ya kitaifa kwaajili ya maendeleo ya takwimu na katika mipango ya kazi ya Kikanda. 
Akielezea zaidi mchango wa ICT katika eneo zima la ukusanyaji wa Takwimu na umuhimu wake katika utekelezaji wa malengo mbalimbali ya maendeleo Barani Afrika, Dkt. Albina Chuwa anasema ukusanywaji wa takwimu katika ngazi za kitaifa lazima uimarishwe kwa kuweka utaratibu wa uratibu kati ya taasisi husika pamoja na Ofisi za Taifa za Takwimu. Kuhusu uwezeshaji, Mkurugenzi Mkuu amesema, Afrika inahitaji kuimarisha uwezo wake wa kutafuta rasilimali ndani ya Afrika , ili hatimaye Afrika ijijengee uwezo wa kuboresha ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa viashiria vya msingi vya ICT katika Afrika. 
Aidha kutokana na ongezeko la matumizi ya ICT katika Afrika, Afrika imeutaka Umoja wa Mataifa, kupitia Kamisheni yake ya Takwimu, kurekebisha taarifa ilizonazo ili ziweze kutoka picha halisi ya maendeleo ya ukuaji wa ICT katika Afrika ikiwa ni pamoja na hatua ambazo zimefikiwa na Bara hilo katika eneo la ICT. 
Katika hatua nyingine, Dkt. Albina Chuwa akichangia katika ajenda iliyohusu utekelezaji wa mfumo wa mazingira ya uhasibu wa kiuchumi ( SEEA) alipendekeza kwamba nchi za Afrika , Tanzania ikiwamo, zitahitaji kuwezeshwa kimafunzo na kiutaalamu ili zijenge uwezo wa kuutumia mfumo huo. 
Akasema Tanzania ingependa kuona wataalamu walioandaa mfumo huo wanakuja na mkakati wa utoaji mafunzo na uwezeshaji kwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania na hasa ikizingatiwa umuhimu wa Takwimu katika utekelezaji wa malengo mbalimbali ya maendeleo baada ya 2015.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya  Takwimu , Dkt. Albina  Chuwa  akiwasilisha hoja  na mchango wa Afrika  wakati wa majadiliano ya ajenda  kuhusu  Teknolojia ya  Habari na Mawasiliano (ICT) katika  Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa unaoendelea hapa Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa. Pamoja na kueleza  namna Afrika  ilivyopiga hatua katika eneo hilo, pia alieleza changamoto ambazo Afrika bado inakabiliana nazo.   Aliyekaa kiti cha  nyuma ni  Bibi.  Aldegunda Komba,  Kaimu Mkurugenzi wa  Shughuli za Takwimu
 Hajjat Amina Mrisho Said,  Kamishna wa Sensa,  na  Bw. Wilfred Mwingira,  Meneja wa  Shughuli za Takwimu wakifuatilia  majadiliano ya  Mkutano wa  45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa,  Mkutano huu  unawakutanisha  wataalamu wa takwimu kutoka nchi 24 ambazo ni wajumbe wa Kamisheni pamoja na wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa.  Mkutano  huu  unafanyika katika  kipindi ambacho tayari kuna  majadiliano ya wazi  yanayoendelea ya kikosi kazi  kinachoandaa ajenda  mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015.   Nafasi na  umuhimu wa suala la Takwimu katika utekelezani wa malengo ya maendeleo  ni jambo ambalo  limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika majadiliano  hayo.
Mjumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tisa wa majadiliano kuhusu ajenda mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015, Dkt. Lorah Madete   akijiandaa kutoa mchango wa Tanzania katika  mkutano wa pamoja kati ya wajumbe wa kikosi  kazi   k uhusu ajenda mpya za  SDGs baada ya 2015 na  Kikundi cha Wataalam ambao wamekuwa wakijadiliana na kuangalia namna gani au ni kwa vipi malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu  baada ya 2015 yatafadhiliwa au kuwezeshwa kwa maana  ya rasilimali fedha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...